Posts

Showing posts from November, 2024

KAGERA SUGAR YAICHAPA DODOMA JIJI 2-1 KAITABA

Image
TIMU ya Kagera Sugar imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mabao ya Kagera Sugar yamefungwa na kiungo Mganda, Peter Lwasa dakika ya 19 na mshambuliaji Kassim Ibrahim Fekha dakika ya 23, wakati bao pekee la Dodoma Jiji limefungwa na kiungo Zidane Ally Sereri dakika ya 45’+2. Kwa ushindi huo, Kagera Sugar inafikisha pointi nane katika mchezo wa 10, ingawa inabaki nafasi ya 14, wakati Dodoma Jiji inabaki na pointi zake 13 za mechi 11 sasa nafasi ya tisa.

CHUKWU AFUNGA PENALTI TABORA UNITED YAILAZA MASHUJAA 1-0 MWINYI

Image
WENYEJI, Tabora United wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Mashujaa FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Bao pekee la Tabora United limefungwa na kiungo mlinzi, Morice Ugochukwu Chukwu raia wa Nigeria kwa penalti nane ya mchezo huo. Kwa ushindi huo Tabora United wanafikisha pointi 14 na kusogea nafasi ya saba, wakiishushia nafasi ya nane Mashujaa inayobaki na pointi zake 13 baada ya wote kucheza mechi 10.

TANZANIA PRISONS YAWAKANDA KEN GOLD 1-0 SOKOINE

Image
TIMU ya Tanzania Prisons imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya ndugu zao, Ken Gold katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Sokoine Jijini Mbeya.  Bao la Tanzania Prisons leo limefungwa na Jumanne Elfadhili Nimkaza kwa penalti dakika ya 52 na kwa ushindi huo inafikisha pointi 10 katika mchezo wa 10 na kusogea nafasi ya 12. Kwa upande wao Ken Gold waliopanda Ligi Kuu msimu huu wanabaki na pointi zao tano za mechi 11 sasa wakiendelea kushika mkia kwenye ligi ya timu 16.

SINGIDA BLACK STARS YAAMBULIA SULUHU KWA COASTAL UNION

Image
TIMU ya Singida Black Stars jana ililazimishwa sare ya bila mabao na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Matokeo hayo yanaifanya Black Stars ifikishe pointi 23 katika mchezo wa 10 na inabaki nafasi ya pili ikizidiwa pointi moja na mabingwa watetezi, Yanga ambao pia wana mechi moja mkononi, wakati Coastal Union inafikisha pointi 12 katika mchezo wa 11 nafasi ya tisa.

AZAM FC YAINYAMAZISHA YANGA, YAICHAPA 1-0 SILLAH AMTUMGUA DIARRA

Image
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya mabingwa watetezi, Yanga SC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, winga Mgambia, Gibril Sillah dakika ya 33 akimalizia pası ya kiungo mzawa, Adolf Mtasingwa Bitegeko. Yanga walifungwa bao hilo wakiwa pungufu uwanjani baada ya refa Ahmed Arajiga wa Manyara kumtoa nje kwa kadi nyekundu beki Ibrahim Abdallah Hamad ‘Bacca’ dakika ya 21 kufuatia kumchezea rafu mshambuliaji wa Azam FC, Nassor Saadun Hamoud. Kwa ushindi huo, Azam FC wanafikisha pointi 21 katika mchezo wa 10, ingawa inabaki nafasi ya nne, wakati Yanga inabaki na pointi 24 za mechi tisa sasa ikiendelea kuongoza Ligi Kuu.

MASHUJAA FC 0-1 SIMBA SC (LIGI KUU YA NBC TZ BARA)

Image
 

MUKWALA AFUNGA DAKİKA YA MWISHO SIMBA YAICHAPA MASHUJAA 1-0 KIGOMA

Image
SIMBA SC imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Mashujaa katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Uganda, Steven Dese Mukwala dakika ya 90’+6 akiunganishwa kwa kichwa kona iliyochongwa na kiungo mzawa mwenye rasta kama yeye, Awesu Ally Awesu. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 22 na kupanda nafasi ya pili ikiizidi tu wastani wa mabao Singida Black Stars baada ya wote kucheza mechi tisa, wakati Mashujaa inabaki na pointi zake 13 za mechi tisa pia nafasi ya saba.