Posts

Showing posts from January, 2025

MZIZE MCHEZAJI BORA, RAMOVIC KOCHA BORA LIGI KUU DESEMBA 2024

Image
MSHAMBULIAJI wa Yanga, Clement Francis Mzize ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara mwezi Desemba 2024, huku Kocha wake, Mjerumani Siad Ramovic akishinda Tuzo ya Kocha Bora mwezi huo wa kufungia mwaka.

SIMBA SC YAWATANDIKA WAALGERIA 2-0 KIBU NA ATEBA

Image
WENYEJI, Simba SC wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya CS Constantine ya Algeria katika mchezo wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC leo yamefungwa na kiungo mzawa, Kibu Dennis Prosper dakika ya 61 na mshambuliaji Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida dakika ya 79. Kwa ushindi huo, Simba SC inafikisha pointi 13 na kumaliza kileleni mwa kundi hilo, mbele ya CS Constantine yenye pointi 12 na zote zimefuzu Robo Fainali. Mechi nyingine ya Kundi A Kombe la Shirikisho leo wenyeji, CS Sfaxien wameichapa Bravos do Maquis Uwanja wa Olimpiki Hammadi-Agrebi mjini Radès, Tunisia. Pamoja na kipigo cha leo Bravos do Maquis wamemaliza nafasi ya tatu kwa pointi zao saba, huku Sfaxien yenye pointi tatu imeshika mkia.  

YANGA WAIKOSA ROBO FAINALI LIGI YA MABINGWA

Image
SAFARI ya Yanga katika Ligi ya Mabingwa Afrika imeishia hatua ya 16 Bora baada ya kumaliza nafasi ya tatu kwenye Kundi A kufuatia sare ya bila mabao na MC Alger katika mchezo uliofanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Yanga ilihitaji ushindi leo ili kufuzu kwa mara ya pili mfululizo Robo Fainali, lakini mpango mzuri wa kujilinda wa MC Alger na papara za wachezaji wake kila walipopata nafasi ziliwanyima mabao wenyeji. Mechi nyingine ya mwisho ya Kundi A leo, wenyeji TP Mazembe wameibuka na ushindi wa 4-0 dhidi ya Al Hilal Omdurman Jijini Lubumbashi, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Kwa matokeo hayo, Al Hilal Omdurman imemaliza kileleni na pointi zake 10, ikifuatiwa na MC Alger pointi tisa na zote zimefuzu Robo Fainali, wakati Yanga yenye pointi nane na Mazembe pointi tano zote zimeaga.

RAIS MWINYI AWAZAWADIA SH MILIONI 50 WACHEZAJI ZANZIBAR HEROES

Image
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Hassan Mwinyi ameizawadia Timu ya Taifa ya Zanzibar, Zanzibar Heroes Shilingi Milioni 50 baada ya kutwaa Kombe la Mapinduzi 2025. Akizungumza  katika Hafla Maalum ya Chakula cha Mchana aliyoiandaa kwa ajili ya Wachezaji wa Timu hiyo katika Viwanja Vya Ikulu, Rais Dk, Mwinyi  ameeeleza kuwa  timu hiyo imeiletea Heshima kubwa Zanzibar na Kudhihirisha Kuwa kuna Vipaji vingi vya Soka hapa nchini vinavopaswa Kuendelezwa katika Maeneo mbalimbali.. Dk,,Mwinyi  Amefahamisha kuwa  kwa Mafanikio ya  Zanzibar Heroes kuna  kila sababu  kwa Serikali  Kuendelea na UjenzI wa Academy za Soka Kila Mkoa  kwa Lengo la.Kuviibua Vipaji vya Vijana. Rais Dk, Mwinyi ametangaza Dhamira  ya Kuunda Kamati Maalum ya Kitaifa hivi  karibuni itakayokuwa na Jukumu la  Kumshauri Namna Bora ya  kuuendeleza Mpira wa Miguu hapa nchini. Dk. Mwinyi ameeleza kuwa Hatua za Timu za...

YANGA YAFUNGA DIRISHA DOGO KWA USAJILI WA JONATHAN IKANGALOMBO KAPELA

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha winga wa kulia, Jonathan Ikangalombo Kapela kutoka AS Vita Club ya kwao, Kinshasa, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa mchezaji wake mpya wa pili dirisha hili dogo. Anamfuatia beki wa kulia, Israel Patrick Mwenda anayeweza kucheza kama winga wa kulia pia na kiungo, aliyesajiliwa kwa mkopo wa hadi mwisho wa msimu kutoka Singida Black Stars.

TANZANIA YAPANGWA KUNDI LA KAWAIDA CHAN, KENYA SHUGHULI WANAYO, UGANDA…

Image
WENYEJI wenza, Tanzania wamepangwa Kundi B katika Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN)  pamoja na Madagascar, Mauritania, Burkina Faso na Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR). Katika droo iliyofanyika usiku wa leo ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya – wenyeji wenza wengine, Kenya wamepangwa Kundi B pamoja na mabingwa mara mbili wa CHAN, Morocco, Angola, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na  Zambia. Wenyeji wenza wengine, Uganda wamepangwa Kundi C pamoja na Niger, Guinea na timu nyingine mbili zitakazojulikana baadaye na Kundi D linazikutanisha Senegal, Kongo-Brazzaville, Sudan na Nigeria. Droo hiyo iliondeshwa na Mkurugenzi wa Mashindano wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF,) Samson Adamu aliyesaidiwa na wachezaji wastaafu, McDonald Mariga wa Kenya, Mrisho Ngasa wa Tanzania na Hassan Wasswa wa Uganda. Michuano hiyo ya nane ya awali ilikuwa ifanyike Februari, lakini imesogezwa mbele hadi Agosti ili kutoa fursa kwa w...

M-BET YATAMBULISHA TOVUTI YENYE HUDUMA BORA NA BOMBA KWA WATEJA

Image
Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Levis Paul akizungumza wakati wa utambulisho mpya wa tovuti ya kampuni hiyo ambayo imeboreshwa na kuwa ya kisasa na kuwawezesha  watejawao kubashiri KAMPUNI inayojulikana kwa ubunifu katika sekta ya michezo ya kubahatisha, M-Bet Tanzania, imezindua muonekano mpya wa tovuti yake kwa lengo la kuboresha huduma kwa wateja.  Tovuti hiyo, inayopatikana kupitia www.m-bet.co.tz, inawawezesha wateja kubashiri aina mbalimbali za michezo na kufanya miamala ya kuweka na kutoa fedha kwa urahisi zaidi. Kupitia tovuti hiyo pia unaweza kucheza Aviator na defender bila ya kwenda Casino. Meneja Masoko wa M-Bet Tanzania, Levis Paul, amesema  kuwa uboreshaji huo ni hatua ya kuthamini wateja na kuwapa huduma bora zaidi ambapo ili kujiunga unajisajili kwenye tovuti hiyo www. m-bet.co.tz na kufuata maelelezo ambapo kwa wateja wa zamani, wanatakiwa kujiunga na kuingiza neno siri (password) upya. "Mbali na kuwa na odds kubwa, tumeamua kuboresha tovu...

CAF YASOGEZA MBELE FAINALI ZA CHAN ILI MAANDALIZI YAKAMILIIKE VIZURI

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) jana lilitangaza kuahirisha Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) 2024 zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi za Kenya, Tanzania na Uganda  hadi Agosti 2025. Taarifa ya CAF ilisema wenyeji, Kenya, Tanzania na Uganda wamefanikisha vizuri zoezi la ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya kufanyia mazoezi, hoteli, hospitali na miundombinu na vifaa vingine kwa ajili ya kuandaa Fainali za CHAN. Hata hivyo, wataalam wa Ufundi na Miundombinu wa CAF ambao baadhi yao wamejikita katika nchi za Kenya, Tanzania na Uganda, wameishauri CAF kuwa muda zaidi unatakiwa kuhakikisha miundombinu na vifaa viko katika viwango vinavyohitajika kwa ajili ya kufanya CHAN yenye mafanikio. Rais wa CAF, Dk Patrice Motsepe alisema: “Napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa Rais William Ruto wa Kenya, Rais Samia Suluhu Hassan wa Tanzania na Rais Yoweri Museveni wa Uganda kwa uongozi wao, kujitolea na maendeleo mazuri yaliyofikiwa katika kujenga na kuboresha viwanj...

SIMBA KUIKABILI CS CONSTANTINE UWANJA MTUPU BILA MASHABIKI

Image
SHIRIKISHO la Soka Afrika (CAF) limeifingia klabu ya Simba kuingiza watazamaji katika mechi zake mbili za Kombe la Shirikisho Afrika baada ya vurugu zilizotokea kwenye mechi dhidi ya CS Sfaxien ya Tunisia Desemba 15, 2024 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Siku hiyo, Simba SC ilitoka nyuma na kushinda 2-1 kabla ya vurumai kuibuka na mashabiki wake kushambuliana na mashabiki wa wageni kwa kurushiana viti walivyokuwa wanang’oa uwanjani. Maana yake Simba hawatakuwa na watazamaji katika mchezo wao wa mwisho wa Kundi A Kombe la Shirikisho dhidi ya CS Constantine Jumapili.

NI ZANZIBAR HEROES BINGWA KOMBE LA MAPINDUZI

Image
WENYEJI, Zanzibar wamefanikiwa kutwa Kombe la Mapinduzi ya Zanzibar baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Burkina Faso usiku wa leo Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar. Mabao ya Zanzibar Heroes yamefungwa na Ibrahim Hamad ’Hilika’  dakika ya 41 na Hassan Ali dakika ya 90’+2, wakati la Burkina Faso limefungwa na Abuobacar Traore dakika ya 69.

MRISHO NGASSA, WASSWA WA UGANDA NA MARIGA KUCHEZESHA DROO YA CHAN

Image
NYOTA wa zamani wa soka Afrika Mashariki, Hassan Wasswa wa Uganda, Mrisho Ngassa wa Tanzania na McDonald Mariga wa Kenya wameteuliwa kuwa Wasaidizi wa Droo ya upangaji wa Ratiba ya Fainali za Michuano ya Ubingwa wa Mataifa ya Afrika (CHAN) Jumatano. Droo hiyo ya Fainali hizo zinazoandaliwa kwa pamoja na nchi Kenya, Tanznaia na Uganda zitakazofanyika kuanzia Februari 1 hadi 28 itafanyika Jumatano kuanzia Saa 11:00 jioni ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Kenyatta (KICC) Jijini Nairobi, Kenya.  Timu zilizofuzu kushiriki Fainali hizo pamoja na wenyeji, Kenya na Tanzania na Uganda - nyingine ni Morocco, Sudan, Niger, Jamhuri ya Afrika ya Kati (CAR), Zambia, Burkina Faso, Guinea, Nigeria, DRC, Rwanda, Angola, Senegal, Madagascar, Kongo Brazzaville na Mauritania.

YANGA YAICHAPA AL HILAL 1-0 MAURITANIA

Image
KLABU ya Yanga imeweka hai matumaini ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al-Hilal Omdurman ya Sudan leo Uwanja wa Cheikha Ould Boidiya Jijini Nouakchott nchini Mauritania. Bao pekee la Yanga katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo mshambuliaji wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya saba baada ya kupokea pasi ya beki Dickson Nickson Job. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi saba, ingawa inabaki nafasi ya tatu nyuma ya Al Hilal yenye pointi 10 na MC Alger ya Algeria pointi nane, wakati TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemolrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi mbili inashika mkia.  Mechi za mwisho Yanga watakuwa wenyeji wa MC Alger Jumamosi ijayo kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa Benjamin Mkapa na mshindi wa mchezo huo afaungana na Al-Hilal Omdurman kwenda Robo Fainali. Kwa MC Alger hata sare itawasogeza hatua inayofuata ya michuano hiyo.

AZAM FC YAMSAJILI CHIPUKIZI 'FUNDI WA MPIRA' ZIDANE SERERI

Image
KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo mshambuliaji, Zidane Sereri (19) kutoka Dodoma Jiji kuwa mchezaji wake mpya kwa mkataba wa miaka mitano utakaodumu hadi mwaka 2030. Huyo anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa Azam FC dirisha hili dogo baada ya beki Zouzou Landry kutoka AFAD Djekanou ya kwao, Ivory Coast. Zouzou Landry, mwenye umri wa miaka 23 tu, anayecheza nafasi za beki wa kushoto na wa kati — amesaini mkataba wa miaka minne, utakaodumu hadi mwaka 2028. 

ZANZIBAR HEROES YATINGA FAINALI KOMBE LA MAPINDUZI, HARAMBEE STARS ‘OUT’

Image
WENYEJI, Zanzibar wamefanikiwa kutinga Fainali ya Kombe la Mapinduzi baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Kenya usiku huu Uwanja wa Gombani kisiwani Pemba. Bao pekee la Zanzibar Heroes lililokatisha safari ya Harambee Stars kwenye michuano hiyo iliyoshirikisha timu nne limefungwa na Ali Khatib ‘Inzaghi’ dakika ya 90’+3 akimalizia kazi nzuri ya Nahodha, Feisal Salum ‘Fei Toto’. Timu zote mbili zilimaliza pungufu baada ya wachezaji wawili kutolewa kwa kadi nyekundu, Abdu Omar wa Harambee Stars dakika ya 68 na Ibrahim Ame wa Zanzibar Heroes dakika ya 90’+9. Kwa ushindi huo, Zanzibar Heroes inafikisha pointi sita na kumaliza nafasi ya pili, nyuma ya Burkina Faso yenye pointi saba na Kenya pointi nne, wakati Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars’ imetoka patupu kufuatia kufungwa mechi zote tatu. Sasa Burkina Faso na Zanzibar zitakutana katika mchezo wa Fainali Jumatatu hapo hapo Uwanja wa Gombani. 

TANZANIA BARA ‘KICHWA CHA MWENDAWAZIMU’ KOMBE LA MAPINDUZI

Image
TIMU ya Tanzania Bara imekamilisha mechi zake tatu za Kombe la Mapinduzi kwa kupoteza zote baada ya leo pia kuchapwa mabao 2-0 na Burkina Faso Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar. Mabao yaliyoiteketeza Kilimanjaro Stars leo yamefungwa na Abdoulkarim Baguian dakika ya 30 na Clement Pitroipa dakika ya 42 na kwa ushindi huo The Stallions inafikisha pointi saba na kuendelea kuongoza ligi ya michuano hiyo. Kenya ‘Harambee Stars’ inafuatia nafasi ya pili kwa pointi zake nne, ikifuatiwa na wenyeji, Zanzibar wenye pointi tatu. Zanzibar Heroes na Harambee Stars watakamilisha Hatua ya awali ya michuano hiyo kwa mchezo baina yao utakaoanza Saa 1:15 usiku hapo hapo Uwanja wa Gombani. Ikumbukwe mshindi wa kwanza na wa pili ndio watakaokutana katika Fainali Januari 13, hapo hapo Uwanja wa Gombani.

AZAM FC YASAJILI BEKI MPYA MUIVORY COAST ANAITWA ZOUZOU

Image
KLABU ya Azam FC imemtambulisha beki Zouzou Landry kutoka AFAD Djekanou ya Ivory Coast kuwa mchezaji wake wa kwanza mpya katika dirisha dogo la usajili wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Zouzou Landry, mwenye umri wa miaka 23 tu, anayecheza nafasi za beki wa kushoto na wa kati — amesaini mkataba wa miaka minne, utakaodumu hadi mwaka 2028. 

KILIMANJARO STARS YATOLEWA MAPEMA KOMBE LA MAPINDUZI PEMBA

Image
TIMU ya Tanzania Bara imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Mapinduzi baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Kenya leo Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar. Mabao ya Harambee Stars yaliyoizamisha Kilimanjaro Stars yamefungwa na Boniphace Muchiri dakika ya 56 na Ryan Ogam dakika ya 68. Kwa ushindi huo, Harambee Stars inafikisha pointi nne, sawa na Burkina Faso, zikifuatiwa na wenyeji, Zanzibar Heroes yenye pointi tatu, wakati Tanzania Bara haina lolote wala chochote baada ya timu zote kucheza mechi mbili mbili.

ZANZIBAR HEROES YACHAPWA 1-0 NA BURKINA FASO KOMBE LA MAPINDUZI

Image
WENYEJI, Zanzibar usiku wa Jumatatu wamechapwa bao 1-0 na Burkina Faso katika michuano ya Kombe la Mapinduzi inayoendelea Uwanja wa Gombani, Pemba, Zanzibar. Bao pekee la The Stallions lililoizamisha Zanzibar Heroes usiku wa jana lilifungwa na Hanabi Hadalou dakika ya 74 na sasa Burkina Faso inaongoza ligi ya michuano hiyo kwa pointi zake nne kuelekea mechi yake ya mwisho na Tanzania Bara. Zanzibar Heroes wanabaki nafasi ya pili kwa pointi zao tatu walizovuna kwenye ushindi wa 1-0 dhidi ya ndugu zao, Kilimanjaro Stars kwenye mchezo wa ufunguzi. Michuano hiyo inaendelea leo kwa mchezo mwingine mmoja, Tanzania  Bara dhidi ya jirani zao, Kenya. Wakati Kilimanjaro Stars ilichapwa 1-0 na Zanzibar Heroes kwenye mechi ya ufunguzi — Harambee Stars waliÅ‚azimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na The Stallions.

SIMBA SC YAICHAPA SFAXIEN 1-0 TUNISIA BAO LA AHOUA

Image
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, CS Sfaxien katika mchezo wa Kundi A Kombe la Shirikisho Afrika leo Uwanja wa Olympique Hammadi-Agrebi mjini Radès nchini Tunisia. Bao pekee la Simba katika mchezo wa leo limefungwa na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast Jean Charles Ahoua dakika ya 34. Kwa ushindi huo, Simba SC imefikisha pointi tisa na kupanda kileleni mbele ya Bravos do Marquis ya Angola na CS Constantine ya Algeria zenye pointi sita kila moja, wakati CS Sfaxien inabaki mkiani kwa rekodi ya kupoteza mechi nne, mbili nyumbani na mbili ugenini. 

MZIZE AFUNGA MAWILI, AZIZ KI MOJA YANGA YAICHAPA TP MAZEMBE 3-1

Image
WENYEJI, Yanga wameweka hai matumaini ya kufuzu Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika mchezo wa Kundi A jioni ya leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Haikuwa ushindi mwepesi kwa mabingwa hao wa Tanzania, Yanga baada ya TP Mazemba, mabingwa mara tano wa michuano kuanza kupata bao dakika ya 16 likifungwa na kipa Msenegal, Alioune Badara Faty kwa penalti kufuatia beki Mkongo, Chadrack Issaka Boka kumchezea rafu beki wa Kimataifa wa Mauritania, Ibrahima Keita mzaliwa wa Mali. Ikawa siku nzuri kwa mshambuliaji mzawa, chipukizi wa umri wa miaka 20, Clement Francie Mzize aliyefunga mabao mawili dakika ya 33 na 60, huku bao lingine la Yanga likifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Burkina Faso, Stephane Aziz Ki dakika ya 56. Kwa ushindi huo, Yanga inafikisha pointi nne na kusogea nafasi ya tatu, ikiishushia nafasi ya nne TP Mazembe inayobaki na pointi zake mbili baada y...

ZANZIBAR HEROES YAICHAPA STARS 1-0 KOMBE LA MAPINDUZI

Image
BAO la kiungo Feisal Salum Abdallah dakika ya 52 limetosha kuipa Zanzibar Heroes ushindi wa 1-0 dhidi ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro Stars katika mchezo wa ufunguzi wa Kombe la Mapinduzi leo Uwanja wa Gombani, Pemba.

LIGI YASIMAMA HADI MACHI KUPISHA MICHUANO YA CHAN NA KOMBE LA MAPINDUZI

Image
Ligi Kuu inasimama Simba SC ikiwa kileleni kwa pointi moja zaidi ya mabingwa watetezi, Yanga baada ya timu zote kucheza mechi 15. BODI ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) imesema kwamba Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara inasimama baada ya mechi za Desemba 29, 2024 kupisha Fainali za michuano ya Ubingwa wa Mataifa wa Afrika (CHAN) ambazo Tanzania itakuwa mwenyeji kwa kushirikiana na Kenya na Uganda. Taarifa ya Bodi ya Ligi jana imesema kwamba kabla ya CHAN michuano ya Kombe la Mapinduzi itaanza Januari 3, 2025 Zanzibar, hivyo Ligi Kuu itasimama hadi Machi Mosi mwaka 2025 itakaporejea na itahakikisha inafikia tamati ndani ya muda wa Kalenda ya msimu. #   Team P W D L F A D P Last 5 matches H2H 1 Simba 15 13 1 1 31 5 +26 40 W W W W W 2 Young Africans 15 13 0 2 32 6 +26 39 W W W W W 3 Azam 16 11 3 2 25 8 +17 36 W W L W W 4 Singida Black … 16 10 3 3 22 11 +11 33 L W W W L 5 Tabora United 15 7 4 ...