Posts

Showing posts from July, 2024

SIMBA SC WAREJEA DAR TAYARI KWA SIMBA DAY JUMAMOSI

Image
KIKOSI cha Simba SC kimerejea nchini jioni ya leo kikitokea Misri ambako kilikuwa kimeweka kambi ya wiki tatu kujiandaa na msimu mpya chini ya kocha wao mpya, Fadlu Davids raia wa Afrika Kusini. Baada ya kutua Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JINIA), eneo la Kipawa Jijini Dar es Salaam – moja kwa moja moja kikosi cha Simba kilikwenda kambini Bunju kwa matayarisho ya mwisho ya tamasha la Simba Day Jumamosi Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini. Simba Day ni tamasha maalum kwa klabu hiyo kutambulisha kikosi cha msimu mpya pamoja na benchi la Ufundi, ambalo hutanguliwa na burudani mbalimbali ikiwemo muziki na Jumamosi hii litahitimishwa kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya APR ya Rwanda. Ikiwa kambini mjini Ismailia nchini Misri – Simba Sports Club ilipata mechi tatu za kujipima nguvu na kushinda zote, 3-0 dhidi ya El-Qanah Julai 22 na 2-1 mara mbili, dhidi ya Telecom Egypt Julai 28 na dhidi ya Al-Adalah FC ya Saudi Arabia Julai 29. Baada ya tamasha la Simba Day, Wekundu hao wa

BEKI WA YANGA PRINCESS AJIUNGA NA TIMU YA ISRAEL

Image
BEKİ chipukizi wa Kimataifa wa Tanzania, Noela Patrick Luhala (18) amejiunga na klabu ya ASA Tel Aviv WFC ya Ligi Kuu ya Wanawake Israel akitokea Yanga Princess ya nyumbani, Dar es Salaam.

TANZANIA YAPOTEZA MWANAMICHEZO WA PILI PARIS OLIMPIKI 2024

Image
KARATA ya pili ya Tanzania katika mashindano ya Olimpiki ya Paris 2024 imeingia maji leo wakati muogeleaji Collins Phillip Saliboko, alipomaliza katika nafasi ya saba alipojitosa katika bwawa la Paris les Defence Arena na kupambana na ushindani mkali sana katika michuano ya mita 100 (Freestyle) kwa wanaume. Saliboko ametumia sekunde 53:38  kumaliza mchuolano huo, wakati mshindi wa kwanza Ovesh Purahoo kutoka  Mauritius ametumia sekunde 52:22, ikiwa ni tofauti ya sekunde 1:16 tu. Mhe Waziri ambaye ameshuhudia mwenyewa mchuano huo, amempongeza Saliboko mwenye umri wa miaka 22 kwa juhudi zake ambazo zimemuwezesha kuvunja rekodi yake mwenyewe ya sekunde 52: 54 aliyoiweja kwenye mashindano ya Jumuiya ya Madola mwaka 2022. Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Dkt Dam as Ndumbaro amemtaka Saliboko, aendeleze juhudi za kufanya mazoezi ili aendelee kuwakilisha nchi katika mashindano makubwa yajayo. Amemwambia Saliboki anayesoma University of Indianapolis, Marekani kwanba kwa umri aliona

'KAPTENI' OPA CLEMENT AJIUNGA NA HENAN FC YA LIGI KUU YA CHINA

Image
MSHAMBULIAJI wa Kimataifa wa Tanzania, Opah Clement Tukumbuke (23) amejiunga na timu ya Henan Wanxian Mountain WFC inayoshiriki Ligi Kuu ya Wanawake China akitokea Beşiktaş ya Uturuki.  Nahodha wa timu ya taifa ya soka ya wanawake, ‘Twiga Stars’ anajiunga na timu hiyo baada ya uzoefu wa kucheza Ligi Kuu ya Uturuki katika klabu za Besiktas na Kayseri Kaddin. Pamoja na Opa, imesajili wachezaji wengine wapya watatu kuimarisha kikosi chake kuelekea msimu ujao wa Ligi ya Wanawake China – wengine ni Zhijie, Chen Lingling na Zhang Wei.

AZAM FC YAPEWA SOMO KWA VITENDO MOROCCO, YACHAPWA 4-1 WYDAD AC

Image
TIMU ya Azam FC imechapwa mabao 4-1 na wenyeji, Wydad Athletic FC katika mchezo wa kirafiki uliofanyika usiku wa jana Uwanja wa El Bacchir mjini Mohammedia nchini Morocco. Mabao ya Wydad yamefungwa na washambuliaji Mohamed Rayhi, Mounir El Habach, Chouaib Fardi na Mohamed El Ouardi, wakati bao pekee la Azam FC limefungwa na beki Msenegal, Cheikh Sidibé kwa penalti. Huo unakuwa mchezo wa tatu wa kirafiki katika kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Morocco baada ya Julai 20 kushinda 3-0 dhidi ya wenyeji wengine, Union Yacoub El Mansour na Julai 27 kutoa sare ya 1-1 na wenyeji, Union de Touarga. Azam FC ambayo msimu ujao pamoja na mashindano ya nyumbani pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika - sasa itarejea nchini mapema Agosti na kuunganisha safari kwenda Rwanda kucheza na wenyeji, Rayon Sports katika mchezo mwingine wa kirafiki. Azam FC inatarajiwa kuuanza msimu mpya kwa mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex, Za

SIMBA SC YAICHAPA 2-1 TIMU YA SAUDI ARABIA MECHI YA KIRAFIKI MISRI

Image
TIMU ya Simba SC imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Al-Adalah FC ya Saudi Arabia katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Suez Canal mjini Ismailia nchini Misri. Mabao ya Simba SC inayofundishwa na Kocha Fadluraghman "Fadlu" Davids raia wa Afrika Kusini yamefungwa na washambuliaji wapya, Mganda Steven Mukwala dakika ya tisa na Mzambia, Joshua Mutale dakika ya 32. Huo unakuwa mchezo wa tatu kwa Simba SC kwenye kambi yao hiyo baada ya Julai 22 kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya El-Qanah na jana kushinda 2-1 dhidi ya Telecom Egypt  Uwanja wa Mercure kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya mjini Ismailia nchini Misri. Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mjini Ismailia nchini Mısri na inatarajiwa kurejea nchini mapema Agosti kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo Simba itarejea Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kumenyana na watani, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.

SIMBA SC YATOKA NA KUICHAPA TELECOM EGYPT 2-1

Image
TIMU ya Simba SC imetoka nyuma na kushinda 2-1 dhidi ya Telecom Egypt katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Mercure kwenye kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya mjini Ismailia nchini Misri.  Mabao ya Simba leo yamefungwa na mshambuliaji mpya, Valentino Mashaka Kusengama aliyesajiliwa kutoka Geita Gold na Ladaki Juma Chasambi. Huo unakuwa mchezo wa pili kwenye kambi yao hiyo baada ya Julai 22 kuibuka na ushindi wa 3-0 dhidi ya El-Qanah, mabao ya viungo, Muivory Coast Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 14 na 16 na Mnigeria,  Augustine Okejepha dakika ya 120. Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mjini Ismailia nchini Mısri na inatarajiwa kurejea nchini mapema Agosti kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo Simba itarejea Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kumenyana na watani, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii.

AZİZ Kİ APIGA MBILI, DUBE MOJA YANGA YATWAA KOMBE LA TOYOTA

Image
MABINGWA wa Tanzania wametwaa taji la kwanza la msimu, Kombe la Toyota baada ya kuwafunga wenyeji, Kaizer Chiefs mabao 4-0 jioni ya leo Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein nchini Afrika Kusini. Mabao ya Yanga yamefungwa na mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 25, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki mawili, dakika ya 45’+3 na 63 na mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize ambaye sasa anatumika kama winga, dakika ya 57. Baada ya mchezo huo, Aziz Ki alitangazwa Mchezaji Bora wa Mechi na kupewa mfano wa hundi ya Randi za Afrika Kusini 5000, zaidi ya Sh. Milioni 7.3 za Tanzania huku Yanga wakikabidhiwa Kombe. Yanga inakamilisha mechi zake za kirafiki katika ziara yake ya wiki mbili Afrika Kusini, nyingine mbili wakifungea 2-1 na Augsburg ya Ujerumani na kushinda 1-0 dhidi ya TS Galaxy mjini Mpumalanga. Mabingwa hao Tanzania sasa wanatarajiwa kurejea nchini kwa ajili ya tamasha la Kilele ch Wiki ya Mwananchi Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es S

AZAM FC YATOA SARE YA 1-1 NA TOUARGA MECHI YA KIRAFIKI MOROCCO

Image
TIMU ya Azam FC jana imelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na wenyeji, Union de Touarga katika mchezo wa kirafiki uliofanyika kwenye Uwanja wa mazoezi mjini Ben Slimane nchini Morocco. Bao la Azam FC limefungwa na mchezaji mpya, mshambuliaji Nassor Saadun Hamoud aliyesajiliwa kutoka Geita Gold na huo unakuwa mchezo wa pili ya kirafiki katika kambi yao ya kujiandaa na msimu mpya nchini Morocco baada ya Julai 20 kushinda 3-0 dhidi ya wenyeji wengine, Union Yacoub El Mansour. Azam FC ambayo msimu ujao pamoja na mashindano ya nyumbani pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika - itakamilisha mechi zake za kirafiki kwenye kambi hiyo Jumatatu kwa kucheza na wenyeji wengine, Wydad Athletic, kabla ya kikosi kurejea nchini mapema Agosti. Azam FC watakuwa na safari ya Rwanda kucheza na Rayon Sports, kabla ya kurejea tena nchini tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

YANGA KUVAA JEZI NYEUSI NA NYEUPE MSIMU UJAO, NYINGINE NI...

Image
KLABU ya Yanga imetambulisha jezi za msimu mpya, kwa mara ya kwanza ikitoa jezi ya rangi nyeusi na nyeupe ambayo itakuwa jezi ya tatu baada ya kijani, dhahabu na bluu  ambayo itakuwa ya nyumbani na njano na kijani ambayo ni ugenini. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

KMC YAWACHAPA WAMAREKANI 5-0 MECHI YA KIRAFIKI MOROGORO

Image
TIMU ya KMC imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Pensacola Christian College Eagles maarufu kama PCC Eagles ya Marekani katika mchezo wa hisani uliofanyika leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro. Mabao ya KMC inayomilikiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni yamefungwa na Ally Shaaban mawili, dakika ya 20 na 56, Kenny Ally mawili pia, dakika ya 25 na 44 na Oscar Paul dakika ya 80.

DODOMA JIJI YAICHAPA SINGIDA BLACK STARS 2-1 ARUSHA

Image
TIMU ya Dodoma Jiji FC leo imetoka nyuma na kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Singida Black Stars katika mchezo wa kirafiki kujiandaa na  msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara uliofanyika Uwanja wa Sheikh Amri Abeid Jijini Arusha. Mabao ya Dodoma Jiji FC yamefungwa na wachezaji wapya, kiungo Ibrahim Ajibu Migomba aliyesajiliwa kutoka Coastal Union dakika ya 52 na Reliants Lusajo Mwakasugule aliyesajiliiwa kutoka Mashujaa ya Kigoma baada ya beki Augustino Samson Nsata kuanza kujifunga dakika ya 14 kuitanguliza Singida Black Stars. 

MNYARWANDA ATAMBULISHWA RASMI MTENDAJI MKUU MPYA SIMBA SC

Image
KLABU ya imemtambulisha Uwayezu Francois Regis kutoka Rwanda kuwa Afisa Mtendaji Mkuu mpya akichukua nafasi ya Imani Kajula anayeachia ngazi mwisho wa mwezi huu.

DABO WA AZAM NA N'DAW WA YANGA WAPO TANGA WANASOMEA UKOCHA

Image
Kocha Mkuu wa Azam FC,Youssoupha Dabo wa Azam FC katika mafunzo ya Kozi ya ukocha ya CAF A Diploma Jijini Tanga.  MAKOCHA Wasenegal, Moussa N'Daw wa Yanga na Youssoupha Dabo wa Azam FC ni miongoni washirikiwa Kozi ya ukocha ya CAF A Diploma inayoendelea kwenye Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mnyanjani Jijini Tanga. Dabo ndiye Mkuu Azam FC, anayesaidiwa na Mfaransa, Bruno Ferry, wakati N'Daw ni kocha Msaidizi Yanga chini ya Muargentina, Miguel Angel Gamondo na wote wawili hawajasafiri na timu zao kwenye kambi za kujiandaa na msimu kwa ajili ya kuhudhuria mafunzo hayo. Kocha Msaidizi wa Yanga, Moussa N'Dawkatika mafunzo ya Kozi ya ukocha ya CAF A Diploma Jijini Tanga.    Ikumbukwe Azam FC imeweka kambi nchini Morocco, wakati Yanga wapo Afrika Kusini na timu zote zitaanza na michuano ya timu, Ngao ya Jamii mapema mwezi ujao. Azam FC itaanza michuano ya Ngao ya Jamii kwa kumenyana na Coastal Union Agosti 8 kuanzia Saa 10:00 jion

HIZI HAPA JEZI ZA MSIMU MPYA SIMBA ZIMEZINDULIWA MIKUMI

Image
KLABU ya Simba imezindua jezi za msimu mpya wa 2024-25, shughuli ambayo imefanyika Hifadhi ya Mikumi mkoani Morogoro ambako mamia ya mashabiki wa timu hiyo walisafiri kwa Treni ya mwendo kasi, SGR kutoka Dar es Salaam kwenda kushuhudia. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 

SIMBA SC KUMCHUKULIA HATUA KIBU DENNIS KWA UTORO

Image
KLABU ya Simba imesema itamchukulia hatua za kinidhamu kiungo wake mshambuliaji, Kibu Dennis Prosper kwa kutoripoti kambini tangu asaini mkataba mpya wa miaka miwili.

AHOUA APIGA MBILI SIMBA SC YASHINDA 3-0 MISRI

Image
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El-Qanah, ambayo pia inajulikana kama Canal SC au Suez Canal katika mechi ya kwanza ya kujipima umbavu kwenye kambi yake ya mjini Ismailia nchini Misri Uwanja wa Old Suez Canal. Mabao ya Simba SC yamefungwa na viungo, Muivory Coast Jean Charles Ahoua mawili, dakika ya 14 na 16 na Mnigeria,  Augustine Okejepha dakika ya 120. Simba SC imeweka kambi ya kujiandaa na msimu mjini Ismailia nchini Mısri na inatarajiwa kurejea nchini mapema Agosti kwa ajili ya tamasha la Simba Day Agosti 3 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Baada ya hapo Simba itarejea Uwanja wa Mkapa Agosti 8 kumenyana na watani, Yanga katika mchezo wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii. GONGA HAPA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

RED ARROWS MABINGWA KOMBE LA KAGAME, AL HİLAL WA TATU

Image
TIMU ya Red Arrows ya Zambia imefanikiwa kutwaa ubingwa wa Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame kwa ushindi wa penalti 10-9  dhidi ya APR ya Rwanda kufuatia sare ya 1-1 ndani ya dakika 120 Leo Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam. Mshambuliaji Ricky Banda alianza kuifungia Red Arrows dakika ya 62, kabla ya mshambuliaji wa Kimataifa wa Mauritania kuisawazishia APR dakika ya 90. Na kwenye mikwaju ya penalti ikawa bahati ya waalikwa kutoka ukanda wa Kusini kwa Afrika (COSAFA) kutwaa taji la michuano hiyo iliyodhaminiwa na Mamlaka ya Bandari Dar es Salaam. Mapema mchana katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu Al Hilal Omdurman ilishinda kwa penalti 3-2 kufuatia sare ya dhidi ya Hay Al Wad Nyala, zote za Sudan hapo hapo Uwanja wa KMC.

AZAM FC YASHINDA 3-0 MECHI YA KIRAFIKI MOROCCO

Image
TIMU ya Azam FC imeibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya wenyeji, Union Yacoub El Mansour ya Ligi Daraja la Tatu Uwanja wa Ziaida Complex mjini Zaida jimbo la Midelt, Drâa-Tafilalet nchini Morocco.  Mabao ya Azam FC yamefungwa na beki Msenegal, Cheikh Tidiane Sidibé, winga Mgambia Gibril Sillah na mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonco Blanco Yus. Azam FC iliyoweka kambi Morocco kujiandaa na msimu mpya, I tashuka tena dimbani Julai 27 kumenyana na Union de Touarga, kabla ya kumenyana na Wydad Athletic Julai 29. Kikosi kitarejea mapema Agosti tayari kwa mchezo wake wa kwanza wa Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii dhidi ya Coastal Union Agosti 8 Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar.

BALEKE AFUNGA YANGA YACHAPWA 2-1 NA AUGSBURG MECHI YA KIRAFIKI AFRIKA KUSINI

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC leo wameanza vibaya michuano ya kuwania Kombe la Mpumalanga International baada ya kuchapwa mabao 2-1 na Augsburg ya Ujerumani Uwanja wa Mbombela, Mpumalanga nchini Afrika Kusini. Mabao ya Augsburg waliomaliza nafasi ya 11 kwenye Ligi ya Ujerumani, Bundesliga msimu uliopita yamefungwa na beki wa kushoto Mdenmark, Mads Pedersen dakika ya 37 na mchezaji mpya, winga wa kushoto Mjapan, Masaya Okugawa dakika ya 80. Bao pekee la Yanga limefungwa na mshambuliaji mpya, Jean Othos Baleke dakika ya 86 akimalizia krosi ya Mkomgo mwenzake, kiungo Maxi Mpia Nzengeli kutoka upande wa kushoto. Yanga SC waliowasili Afrika Kusini Alhamisi kuweka kambi ya kujiandaa na msimu - watateremka tena dimbani Jumatano kumenyana na wenyeji, TS Galaxy, kabla ya kukamilisha mechi zake za kujipima kwa kucheza na Kaizer Chiefs  Jumapili, Julai 28 Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein.

NI APR NA RED ARROWS FAINALI KOMBE LA KAGAME 2024

Image
TIMU za APR ya Rwanda na Red Arrows ya Zambia jana zilifanikiwa kutinga Fainali ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame baada ya kuzitoa Al Hilal Omdurman na Hay Al Wadi Nyala za Sudan Jijini Dar es Salaam. Ilianza APR kuitupa nje Al Hilal Omdurman kwa penalti 5-4 kufuatia sare ya 0-0 ndani ya dakika 120 Uwanja wa KMC, Mwenge Jijini Dar es Salaam, kabla ya Red Arrows kuichapa Hay Al Wadi 2-0, mabao ya Paul Katema dakika ya 117 na Allassane Darra 119 Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini. APR na Red Arrows zitakutana katika Fainali kesho Saa 1:00 usiku Uwanja wa Azam Complex, mchezo ambao utatanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu baina ya Al Hilal Omdurman na Hay Al Wadi.

AZAM FC YAFUNGA USAJILI KWA SAINI YA KIUNGO WA BELOUIZDAD

Image
KLABU ya Azam FC imemsajili kiungo mkabaji wa Kimataifa wa Mali, Mamadou Samake (24) kwa mkataba wa miaka miwili akitokea CR Belouizdad ya Algeria. Taarifa ya Azam FC imesema kwamba Mamadou Samake anafunga rasmi usajili wa klabu hiyo katika dirisha hili la mwanzo wa msimu 2024/25. Taarifa ya Azam FC imesema kwamba Samake atajiunga na kambi ya timu nchini Morocco muda wowote kuanzia sasa, tayari maandalizi ya msimu. Huyo anakuwa mchezaji mpya wa nane baada ya beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na viungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien, kiungo mshambuliaji, Cheickna Diakite (19) kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Real Bamako ya kwao, Mali. Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia. Kuna wazawa pia wawili, kiungo Nassor Saadun Hamoud kutoka Geita Gold na mshambuliaji

KAMPUNI YA MICHEZO YA KUBASHIRI YA BETWINNER YAZINDULIWA RASMI TANZANIA

Image
Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Betwinner, Jesse Ndambala (kushoto) akimkaribisha  Mkurugenzi Mkuu wa Michezo ya Bodi ya Kubahatisha nchini (GBT) James Mbalwe kabla ya uzinduzi rasmi wa kampuni hiyo uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini. KAMPUNI ya michezo ya kubashiri ya Betwinner imezinduliwa rasmi nchini Tanzania, ikileta fursa mpya na za kipekee kwa wateja wa michezo ya kubahatisha. Akizungumza katika hafla ya uzinduzi, Mkurugenzi Mkuu wa Betwinner, Jesse Ndambala, alisema kuwa ujio wao umelenga kuwapa wateja Odds nzuri zaidi kulinganisha na kampuni nyingine za kubashiri. Ndambala alisisitiza kuwa Bet Winner imeleta ubunifu mkubwa katika michezo yao ya kubashiri ikiwa pamoja na kuwapa asilimia 100 ya bonus kwa wateja wapya ikiwa ni sehemu ya ofa ya ukaribisho. "Mbali na kuwa na odds nzuri, tumeweka ubunifu mkubwa katika michezo yetu, na kutoa asilimia 100 ya bonus kwa wateja wapya. Lengo hapa ni kuongeza burudani na chachu ya ushindani kwe

ONANA NA AWESU WAWASILI KAMBINI ISMAILIA SIMBA SC

Image
VIUNGO washambuliaji, Awesu Ally Awesu (28) na Mcameroon Leandre Willy Essomba Onana (24) wamewasili mjini Ismailia nchini Misri  kwenye kambi ya Simba SC kujiunga na wenzao kwa maandalizi ya msimu mpya. Sasa wachezaji wawili tu wanakosekana kwenye kambi ya Simba, beki Lameck Lawi aliyesajiliwa kutoka Coastal Union ya Tanga na kiungo mshambuliaji, Kibu Dennis Prosper. Kuhusu Lawi klabu yake imegoma kumruhusu na suala lao litaamuliwa na Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), wakati Kibu imeripotiwa hajarejea kutoka Marekani alipokwenda kwa mapumziko. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 

YANGA SC WAWASILI SALAMA AFRIKA KUSINI KUIVAA AUGSBURG JUMAMOSI

Image
KIKOSI cha Yanga kimewasili salama jana nchini Afrika Kusini kwa kambi ya kujiandaa na msimu itakayoambatana na mechi kadhaa za kirafiki. Mabingwa hao wa Tanzania wataanza kwa kumenyana na Augsburg ya Ujerumani Jumamosi Uwanja wa Mbombela, Mpumalanga, kabla ya kucheza na wenyeji, Kaizer Chiefs Julai 28 Uwanja wa Toyota mjini Bloemfontein, zote zikirushwa na chaneli ya #AzamSports1HD kuanzia Saa 10:00 jioni. Akizungumza wakati wa safari hiyo, kocha Mkuu wa Yanga, Muargentina Miguel Angel Gamondi amesema kwamba ameridhishwa na namna wachezaji wapya wanavyoendelea kuelewana na wenzao.    Kikosi cha Yanga kinatarajiwa kurejea nchini Julai 30 tayari kwa tamasha la kilele cha wiki ya Mwananchi Agosti 4 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, kabla ya kumenyana na watani, Simba katika Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii Agosti 8.

SIMBA NA YANGA AGOSTI 8 MKAPA NGAO YA JAMII, AZAM NA COASTAL NI ZANZIBAR

Image
MECHI za Nusu Fainali ya Ngao ya Jamii zitachezwa Agosti 8, Azam FC dhidi ya Coastal Union kuanzia Saa 10:00 jioni Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar na Simba dhidi ya Yanga kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Mechi zote za mwisho zitachezwa Agosti 11, ikitangulia ya kusaka mshindi wa tatu Saa 9:00 Alasiri na kufuatiwa na Fainali Saa 1:00 Usiku. Mfumo wa timu nne katika Ngao ya Jamii ulianza rasmi msimu uliopita kwa bingwa wa Ligi Kuu kucheza na mshindi wa tatu, na mshinfi wa pili kumenyana na mshindi wa nne. Simba SC ndio waliokuwa mabingwa msimu uliopita wakiifunga kwa penalti 3-1 dhidi ya watani, Yanga kufuatia sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90, wakati Azam FC ilimaliza nafasi ya tatu baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Singida Fountain Gatew Uanja wa Mkwakwani Jijini Tanga. Simba ilifika Fainali kwa ushindi wa penalti pia 4-2 dhidi ya Singida Fountain Gate huku Yanga wakiifunga Azam FC 2-0.

SABA KUIWAKILISHA TANZANIA OLIMPIKI YA PARIS 2024

Image
KAMATI ya Olimpiki Tanzania (TOC) imetaja wanamichezo saba watakaoiwakilisha Tanzania kwenye Michezo ya Olimpiki ya Paris inayotarajiwa kuanza Julai 26 hadi Agosti 11, mwaka huu. Hao ni pamoja na Wanariadha wanne Alphonce Felix Simbu na Gabriel Geay, wanaume na Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri wanawake, wote mbio ndefu, Marathon. Wengine ni Waogeleaji, Sophia Anisa Latiff 50m freestyle (wanawake) na Collins Phillip Saliboko 100m freestyle (wanaume) na Mcheza Judo, Judo Andrew Thomas Mlugu. Msafara huo uambao utaagwa Ijumaa kabla ya kuondoka Jumapili Alfajiri, utahussha makocha watatu, Daktari mmoja, Maafisa Wawili wa TOC, Mwana Habari mmoja na Mkuu wa Msafara. Kamati ya Olimpiki Tanzania imetoa shukrani za dhati kwa Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Bodi ya Utalii Tanzania (TTB) kwa michango yao kwa timu hiyo.

AISHA MASAKA AJIUNGA BRIGHTON & HOVE ALBION YA ENGLAND

Image
KLABU ya Brighton & Hove Albion imemtambulisha mshambuliaji wa Kimataifa wa Tanzania, Aisha Masaka (20) kutoka BK Hacken ya Sweden kuwa mchezaji wake mpya kwa masharti ambayo hayajawekwa wazi, kulingana na taratibu za kawaida za udhibiti. Mkurugenzi Mkuu wa soka ya wanawake na wasichana wa Brighton & Hove Albion, Zoe Johnson pamoja na kumkaribisha kwa furaha Aisha – pia amemwagia sifa kwamba ni mshambulaji mzuri aliyefanya vizuri katika Ligi ya Sweden na Ligi yaMabingwa Ulaya akiwa na Hacken. Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 20 alijiunga na Hacken mwaka 2022 akitokea Young Africans ‘Yanga Princess’ ya nyumbani, Tanzania baada ya kuibukia Alliance FC ya Mwanza. Katika misimu miwili aliyokaa Hacken, fowadi huyo aliwasaidia kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya Sweden na kuifikisha Robo Fainali ya UEFA Champions League msimu uliopita kabla ya kutolewa na PSG. Wakati anacheza Tanzania, alikuwa Mfungaji Bora msimu wa 2020/21 akiifungia Young Priness jumla ya mabao 35 k

RED ARROWS YATINGA NUSU FAINALI KOMBE LA KAGAME

Image
BAO pekee la Anthony Shipanuka dakika ya 21 jana lilitosha kuipa ushindi wa 1-0 Red Arrows ya Zambia dhidi ya Telecom ya Djobouti katika mchezo wa Kundi Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Uwanja wa KMC, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Mchezo mwingine wa Kundi B jana mabao ya Salah Eldin Adil dakika ya 56 na Mohamed Abdelrahman dakika ya 88 yalitosha kuipa Al Hilal ya Sudan ushindi wa 2-0 dhidi ya Gor Mahia ya Kenya Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Kwa matokeo hayo, Al Hilal inamaliza kileleni na pointi zake tisa, ikifuatiwa na Red Arrows pointi sita, Gor Mahia moja sawa na Telecom. Washindi wa kwanza wa makundi ndio wanakwenda moja kwa moja Nusu Fainali, ambao ni  Hay Al Wadi  Nyala Kundi A,  Al Hilal Omdurman Kundi B, zote za Sudan na APR ya Rwanda Kundi C zikiungana na mshind wa pili bora, Red Arrows. Nusu Fainali zitachezwa Ijumaa APR na Al Hilal Omdurman Saa 10:00 jioni Uwanja wa KMC na Hay Al Wadi dhidi ya Red Arrows Saa 1:0

AZAM FC YASAJILI KIUNGO MSHAMBULIAJI KUTOKA MALİ

Image
KLABU ya Azam FC imemsajili kiungo mshambuliaji, Cheickna Diakite (19) kwa mkataba wa miaka mitatu kutoka Real Bamako ya kwao, Mali. Huyo anakuwa mchezaji mpya wa saba kusajiliwa Azam FC kuelekea msimu ujao, wengine ni beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien. Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia. Kuna wazawa pia wawili, kiungo Nassor Saadun Hamoud kutoka Geita Gold na mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma. Aidha, Azam FC pia imemnunua moja kwa moja na kumsainisha mkataba wa miaka miwili kipa wa Kimataifa was Sudan, Mohamed Mustafa kutoka El Merreikh ya Sudan. Hatua hiyo inafuatia kazi nzuri ya kipa huyo kufuatia kusajiliwa kwa mkopo mwezi Januari akiisaidia Azam FC kumaliza nafasi ya pili kwenye Ligi Kuu ya NBC

SIMBA SC YAACHANA NA PA OMAR JOBE PIA

Image
KLABU ya Simba SC imetangaza kuachana na mshambuliaji wa Kimataifa wa Gambia, Pa Omar Jobe baada ya miezi sita tu tangu awasili Januari mwaka huu kutoka  Zhenis ya Kazakhstan. Huyo anakuwa mchezaji wa tisa kuachwa Simba baada ya mabeki, Mkongo Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Msenegal, Babacar Sarr, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji, Sadio Kanoute wa Mali na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.  Aidha, Simba SC imesajili wachezaji wapya 13, ambao ni mabeki, Kelvin Sospeter Kijiri (24) kutoka Singida Big Stars, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya (DRC), wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union. Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mz

WAZIRI MKUU MAJALIWA APONGEZA UWEKEZAJI MKUBWA AZAM MEDIA KWENYE MICHEZO

Image
WAZIRI Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa jana ameipongeza Kampuni ya Azam Media Limited kwa kuisaidia Tanzania kupata vigezo vya kuwa wenyeji wa Fainali za Kombe la Mataifaya Afrika (AFCON) mwaka 2027. Waziri Mkuu, Majaliwa aliyasema hayo jana wakati wa hafla ya Azam Media Limited kuzindua vifaa vipya na vya kisasa vya kurushia matangazo ya mpira pamoja na mashine za Msaada wa Picha za Video kwa Marefa (VAR), shughuli ambayo ilifanyika Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Waziri Mkuu huyo amelishauri Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) na Azam Media kupitia na kuboresha mikataba yake ya udhamini na Azam Media Limited ili kuwapa uhakika juu ya uwekezaji wao wa Mabilioni ya Fedha. Kwa ujumla Waziri Majaliwa ameipongeza Azam Media kwa kukukuza sekta ya michezo kwa ujumla kutokana na kuonyesha michezo mingi kwenye Televisheni yake mbali na soka - ikiwemo ndondi na mpira wa kikapu.   "Tumekutana hapa kwa ajili ya kushuhudia tukio la kihistoria...n

COASTAL UNION YATOA DROO, SINGIDA YASHINDA KAGAME, LAKINI…

Image
TIMU ya Coastal Union imekamilisha mechi zake za Kundi A Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame kwa kutoa sare ya kufungana bao 1-1 na Hay Al Wadi Nyala ya Sudan Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mohamed Hasssa alianza kuifungia Al Wahdi dakika ya 48, kabla ya Abdallah Dennis kuisawazishia Coastal Union dakika ya 53. Mchezo mwingine wa Kundi A, mabingwa wa Zanzibar, JKU wamechapwa mabao 2-1 na Dekedaha ya Somalia jioni ya leo hapo hapo Uwanja wa KMC. Mabao ya Dekedaha yamefungwa na  Joshua Abdalie dakika ya 60 na Adepoju Oluwasen dakika ya 71, wakati bao pekee la JKU limefungwa na Ahmed Hamisi Machano dakika ya nne. Msimamo wa Kundi A sasa ni  Hay Al Wad pointi saba kileleni wakifuatiwa na Coastal Union pointi nne, JKU pointi tatu sawa na Dekedaha. Mechi za Kundi C zilizochezwa mchana, Singida Big Stars iliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya El Merriekh Bentiu ya Sudan Kusini, wakati SC Villa ya Uganda ililazimishwa sare ya 1-1 na A

IMANI KAJULA AJIUZULU UTENDAJI MKUU SIMBA SC, KUACHIA OFİSİ MWEZI UJAO

Image
AFISA Mtendaji Mkuu wa klabu ya Simba, Imani Kajula amejiuzulu nafasi hiyo baada ya kipindi cha mwaka mmoja na nusu tangu apewe wadhifa huo. Imani Kajula aliteuliwa kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba SC Januari akichukua nafasi iliyoachwa wazi na Barbara Gonzalez aliyejiuzulu Desemba mwaka 2022 kwa notisi ya mwezi mmoja na kuondoka madarakani Januari mwaka jana.

NI HISPANIA BINGWA EURO 2024, YAICHAPA ENGLAND 2-1 UJERUMANI

Image
HISPANIA imefanikiwa kutwaa Kombe la Mataifa ya Ulaya, Euro 2024 baina ya ushindi wa 2-1 dhidi ya England  usiku wa Jumapili Uwanja wa Olympia Jijini Berlin nchini Ujerumani. Nyota mwenye asili ya Ghana, Nicholas ‘Nico’ Williams Arthuer (22) alianza kuwafungia La Roja dakika ya 47 akimalizia pası nzuri ya winga mwenzake mwenye asili ya Afrika,  Lamine Yamal Nasraoui Ebana (17) ambaye baba yake anatokea Morocco na mama yake, Sheila Ebana anatokea Equatorial Guinea. Lakini Cole Jermaine Palmer (22) akaisawazishia Three Lions dakika ya 72 akimalizia pasi ya kiungo mwenzake mshambuliaji, Jude Victor William Bellingham baada ya kazi nzuri ya Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka mwenye asili  Nigeria.Bukayo Ayoyinka Temidayo Saka. Shujaa  wa Hspania leo winga pia, Mikel Oyarzabal Ugarte aliyefunga bao la ushindi dakika ya 86 baada ya kazi nziri ya beki wa Chelsea, Marc Cucurella Saseta. Hilo linakuwa taji la nne kwa Hispania baada ya awali kulitwaa katika miaka ya  1964, 2008 na 2012, wakati

VIJANA SABA WA U20 WAPANDISHWA PRISONS KUBWA

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imepandisha wachezaji saba kutoka timu yake ya vijana chini ya umri wa miaka 20 kwa ajili ya msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Hao ni Kelvin Sengati, Ashraf Mbonde, Erick Mwambenja, Joah Mwakilema, Yohana Mgella, Evance Dalf na Ally Hamza.

AL HILAL YAITANDIKA RED ARROWS 5-0, GOR MAHIA YAAMBULIA SARE KAGAME

Image
TIMU ya Al Hilal FC ya Sudan jana imeibuka na ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Red Arrows FC ya Zambia katika mchezo wa Kundi B Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati, maarufu kama Kombe la Kagame Uwanja wa Azam Comlpex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Al Hilal yalifungwa na Adama Coulibaly matatu, dakika za tisa, 55 na 63 na mengine mawili, Mohamed Abdelathman Yousif dakika ya 14 na 24. Kwa ushindi huo, Al Hilal inafikisha pointi sita kufuatia ushindi wa 2-0 dhidi ya ASAS ya Djibouti katika mchezo wa kwanza, wakati Red Arrows FC inabaki na pointi zake tatu ilizovuna kwenye ushindi wa 1-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Gor Mahia ya Kenya. Mechi nyingine ya Kundi B jana Gor Mahia iliambulia sare ya 1-1 na ASAS hapo hapo Uwanja wa Azam Comlpex. Levin Joseph Odhiambo alianza kuifungia Gor Mahia dakika ya 39, kabla ya Warsama Houssein Said kuisawazishia ASAS dakika ya 41. Baada ya mechi za kwanza, Al Hilal inaongoza Kundi B kwa pointi zake sita, ikifuatiwa na  Red Arrows tatu,

YANGA SC YAAJIRI PHYSIO MOYA KUTOKA AFRİKA KUSINI

Image
KLABU ya Yanga imemtambulisha Sekhwela Silence Seroto, raja wa Afrika Kusini kuwa Mtaalamu wake mpya wa Tiba za Viungo (Physiotherapist).

SIMBA SC YASAJILI BEKI WA KULIA HODARI KELVIN KIJIRI

Image
KLABU ya Simba imemtambulisha beki wa kulia, Kelvin Sospeter Kijiri (24) kutoka Singida Big Stars kuwa mchezaji wake kuelekea msimu ujao. Beki huyo aliyeibukia KMC mwaka 2019, kabla ya kuhamia Singida Big Stars mwaka jana anakuwa mchezaji mpya wa 13 kwenye kikosi cha Wekundu wa Msimbazi.  Wachezaji wengine wapya Simba ni pamoja na mabeki, Mburkinabe Valentin Nouma (24) kutoka FC Saint-Éloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wazawa, Abdulrazack Mohamed Hamza (21) kutoka SuperSport United ya Afrika Kusini na Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union. Wengine ni viungo, Mnigeria, Augustine Okejepha (20) kutoka Rivers United ya kwao, Port Harcourt, Omary Abdallah Omary (23) kutoka Mashujaa FC ya Kigoma, Yusuph Ally Kagoma (28) kutoka Singida Big Stars, Mzambia, Joshua Mutale (22) kutoka Power Dynamos ya kwao, Kitwe, Débora Fernandes Mavambo (24) mwenye uraia pacha wa Kongo - Brazzaville na Angola kutoka Mutondo Stars ya Zambia. Kuna washambuliaji pia, Mganda, Steven

KIKAO KABLA YA KUANZA MAZOEZI AZİZ KI, CHAMA NA PACOME

Image
VIUNGO wanyumbulifu wa Yanga, Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua (kulia), Mzambia Clatous Chota Chama (katikati) na Mburkinabe, Stephane Aziz Ki (Kushiro) wakijadiliana jambo leo wakati wa mazoezi ya timu hiyo Uwanja wa Avic Town, Kigamboni Jijini Dar es Salaam. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 

YANGA KUANZA NA VITAL’O, AZAM NA APR LİGİ YA MABINGWA AFRIKA

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wataanza na Vital’O ya Burundi, wakati Azam FC itaanza na APR ya Rwanda katika Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Yanga itaanzia ugenini na Azam FC itaanzia nyumbani mechi za kwanza zitachezwa kati kati ya Agosti 16 na 18, kabla ya timu hizo kurudiana kati ya Agosti 23 na 25. Kwa upande wao JKU ya Zanzibar wataanzia nyumbani dhidi ya Pyramids ya Mısri. Yanga ikiitoa Vital’O itakutana na mshindi kati ya SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia na Azam FC ikiitoa APR itakutana na mshindi kati ya JKU na Pyramids ya Mısri.

SIMBA SC KUANZA JKU, COASTAL NA WAANGOLA KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
VIGOGO, Simba SC wataanza katika Raundi ya Kwanza ya Kombe la Shirikisho Afrika kumenyana na mshindi kati ya Uhamiaji ya Zanzibar na bingwa wa Kombe la FA ya Libya zitakazomenyana katika Raundi ya Awali. Nayo Coastal Union ya Tanga itaanza ugenini dhidi ya FC Bravos do Maquis ya Angola, ikifanikiwa kuvuka Hatua hiyo itakutana na St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Mechi za kwanza za Raundi ya Awali zitapigwa kati ya Agosti 16 na 18, kabla ya timu hizo kurudiana kati ya Agosti 23 na 25.