Posts

Showing posts from September, 2024

NAMUNGO FC YAZINDUKA NA KUICHAPA COASTAL UNION 2-0 CHAMAZI

Image
TIMU ya Namungo FC imepata ushindi wa kwanza katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuichapa Coastal Union mabao 2-0 jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Namungo FC yamefungwa na Ritch Nkoli dakika ya 38 na Pius Buswita dakika ya 45’+2 huo ukiwa ushindi wa kwanza timu hiyo ikitoka kupoteza mechi tatu mfululizo kwa kufungwa 2-1 na Tabora United, 2-0 na Fountain Gate na 1-0 na Dodoma Jiji . Kwa upande wao Coastal Union wanafikisha mechi tatu bila ushindi, kufuatia awali kutoa sare na KMC 1-1 , kabla ya kufungwa 1-0 na Mshujaa zote Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC Complex), Mwenge Jijini Dar es Salaam.

SINGIDA YA KWANZA KUIFUNGA PAMBA, YAICHAPA 1-0 KIRUMBA

Image
TIMU ya Singida Black Stars imeendeleza wimbi la ushindi katika mchezo wa nne mfululizo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya kuwachapa wenyeji, Pamba Jiji FC bao 1-0 mchana wa leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Bao pekee la Singida Black Stars inayofundishwa na Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems limefungwa na kiungo Mghana, Emmanuel Kwame Keyekeh dakika ya kwanza tu ya mchezo huo. Singida Black Stars inafikisha pointi na kuendelea kuongoza ligi, wakati Pamba Jiji FC iliyo chini ya Kocha Mserbia, Goran Kopunovic inabaki na pointi zake tatu baada ya timu zote kucheza mechi nne.

KAGERA SUGAR YAPATA POINTI YA KWANZA MECHI YA NNE LIGI KUU

Image
WENYEJI, Kagera Sugar wamefikisha mechi nne bila ushindi baada ya leo kuokota pointi ya kwanza kufuatia sare ya bila mabao na JKT Tanzania Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba. Mechi tafu za mwanzo Kagera Sugar ilifungwa 1-0 na Singida Black Stars, 2-0 na Yanga na 1-0 na Tabora United, wakati JKT Tanzania nayo imetoa sare ya pili mfululizo leo katika mechi zake mbili hadi sasa kufuatia sare ya 0-0 na Azam katika mchezo wa kwanza.

KMC YAICHAPA KEN GOLD 1-0 BAO LA REDEMTUS MUSSA

Image
WENYEJI, KMC wameibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya Ken Gold ya Mbeya katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Mwenge Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee Redemtus Mussa kwa shuti la mpira wa adhabu dakika ya 14 na kwa ushindi huo, KMC inafikisha pointi nne katika mchezo wa tatu, wakati Ken Gold inapoteza mechi ya tatu mfululizo kati ya tatu za mwanzo wa msimu ilizocheza.

SIMBA SC YAWABANA AL AHLY KWAO, 0-0 TIPOLI

Image
TIMU ya Simba SC ya bila mabao na wenyeji, Al Ahly Tirpoli usiku huu katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Ijumaa Uwanja wa Juni 11 Jijini Tripoli nchini Libya. Timu hizo zitarudiana Jumapili ya Septemba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam na mshindi wa jumla atakwenda hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.

FOUNTAIN GATE NA DODOMA JIJI ZATOSHANA NGUVU, SARE 2-2 MANYARA

Image
TIMU za Fountain Gate na Dodoma Jiji zimegawana pointi kwa sare ya kufungana mabao 2-2 katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Tanzanite Kwaraa mjini Manyara. Ilikuwa mechi tamu ya funga nikufunge baina ya timu zinazotumia Uwanja wa Tanzanite Kwaraa kama wa nyumbani - mara zote Dodoma Jiji ya kocha Mecky Mexime ikitangulia na Fountain Gate ya kocha Mohamed Muya ikisawazisha. Mabao ya Dodoma Jiji yalifungwa na washambuliaji na Hassan Mwaterema dakika ya 27 na Paul Peter dakika ya 51, wakati ya Fountain Gate waliokuwa wenyeji leo yamefungwa na Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ dakika ya 50 na Dickson Ambundo dakika ya 85. Baada ya mchezo, Suleiman Mwalimu ‘Gomez’ anayecheza kwa mkopo Fountain Gate kutoka Singida Black Stars aliyeuliwa Mchezaji Bora wa Mechi.  Matokeo hayo yanaifanya Fountain Gate ifikishe pointi saba na Dodoma Jiji pointi tano baada ya wote kucheza mechi nne.

CBE SA 0-1 YANGA SC (LIGI YA MABINGWA AFRIKA)

Image
 

SOMOE NG’ITU MWENYEKITI MPYA SOKA YA WANAWAKE TANZANIA

Image
MWANDISHI nguli wa Habari za Michezo nchini, Somoe Robert Ng’itu jana ameshinda Uenyekiti wa Chama cha Soka ya Wanawake Tanzania (TWFA) katika uchaguzi uliofanyika jana Moshi mkoani Kilimanjaro.

AZAM FC YAAMBULIA SULUHU KWA PAMBA JIJI AZAM COMPLEX

Image
WENYEJI, Azam FC wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Pamba Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Ni sare ya tasa ya pili mfululizo katika mechi mbili za mwanzo za msimu kufuatia sare ya 0-0 pia na JKT Tanzania katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni Jijini Dar es Salaam. Na kwa Pamba pia ni mfululizo wa sare tatu za mabao katika mechi tatu za mwanzo za msimu pamoja na zile mbili za nyumbani, Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza dhidi ya Tanzania Prisons na Dodoma Jiji FC.

TABORA UNITED YALAZIMISHWA SARE YA BILA MABAO NA PRISONS NYUMBANI

Image
WENYEJI, Tabora United wamelazimishwa sare ya bila kufungana na Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Matokeo hayo yanaifanya Tabora United ifikishe pointi saba katika mchezo wa nne, wakati Tanzania Prisons inafikisha pointi tatu katika mchezo wa tatu.

YANGA YAICHAPA CBE 1-0 PALE PALE ABEBE BIKILA BAO LA DUBE

Image
KLABU ya Yanga imeibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, timu ya Benki ya Biashara Ethiopia, CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) jioni ya leo katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, mshambuliaji wa Kimataifa wa Zimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya 45’+1 na mchezo wa marudiano utafanyika Jumamosi ya Septemba 21 katika Uwanja ambao utathibitishwa na Yanga. Mshindi wa jumla atakwenda Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.

MECHI YA MARUDIANO YANGA NA CBE KUCHEZWA PEMBA

Image
MCHEZO wa marudiano Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baina ya Yanga na timu ya Benki ya Biashara Ethiopia, CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) utafanyika Uwanja wa Gombani, Pemba Jumamosi ya Septemba 21. Ikumbukwe timu hizo zitamenyana kesho katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa na mshindi wa jumla atakwenda Hatua ya 16 Bora inayochezwa kwa mtindo wa makundi.

NGUSHI APIGA BAO PEKEE MASHUJAA YAICHAPA COASTAL UNION 1-0 MWENGE

Image
BAO la dakika ya 14 la mshambuliaji Crispin Ngushi Mhagmaa limeipa Mashujaa FC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), Mwenge Jijini Dar es Salaam. Kwa ushindi huo, Mashujaa FC wanafikisha pointi saba na kusogea nafasi ya pili, nyuma ya Singida Black Stars yenye pointi tisa baada ya wote kucheza mechi tatu, wakati Coastal Union inabaki na pointi moja kufuatia kucheza mechi mbili.

KANU KUSHIRIKI KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE OKTOBA 14 BUTIAMA

Image
Na Asha Kigundula, Dar es Salaam MWANASOKA Bora wa zamani Afrika, Nwankwo Christian Nwosu Kanu atashiriki maazimisho ya miaka 25 ya kifo cha baba wa Taifa, Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere katika hafla iliyoandaliwa na Kampuni ya Vodacom Tanzania itakayofanyika Oktoba 14, Butiama mkoani Mara. Pamoja na Mwanasoka huyo Bora wa Afrika mara mbili, 1996 na 1999, zaidi ya washiriki 100 wamejiandikisha kushiriki mbio za Baiskeli za 'Twende Butiama'  katika kilele cha kumbukumbu ya hayati baba wa Taifa, Mwalimu. Kanu, aliyetamba klabu za Iwuanyanwu Nationale ya kwao Nigeria, Ajax ya Uholanzi, Inter Milan ya Italia na Arsenal, West Bromwich Albion na Portsmouth za England - amekuja kwa mwaliko wa Taasisi ya Vodacom Tanzania Foundation kwa ajili ya ziara ya mbio za Twende Butiama mwaka 2024.  Kupitia taasisi yake ya Kanu Heart Foundation, Kanu ameelezea kufurahishwa kwake kuungana na juhudi zinazofanywa na Twende Butiama kama sehemu ya kumuenzi Baba wa Taifa wa Tanzania,

SINGIDA BLACK STARS YAENDELEZA UBABE, YAICHAPA KMC 2-1 LITI

Image
WENYEJI, Singida Black Stars wameendeleza wimbo la ushindi katika Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara baada ya jioni ya leo kuichapa KMC mabao 2-1 Uwanja wa CCM Liti mjini Singida. Mabao ya Singida Black Stars inayofundishwa na Kocha Mbelgiji, Patrick Aussems yamefungwa na Josephat Bada dakika ya 40 na Elvis Rupia dakika ya 57, wakati la KMC limefungwa na Redemtus Mussa dakika ya 49. Huo unakuwa ushindi wa tatu kwa Singida Black Star baada ya awali kushinda mechi mbili ugenini dhidi ya Ken Gold 3-1 Jijini Mbeya na Kagera Sugar 1-0 mjini Bukoba. Kwa KMC huo unakuwa mchezo wa pili kucheza bila ushindi, kufuatia kulazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union, nyumbani, Dar es Salaam wiki iliyopita. 

YANGA SC WAIFUATA CBE KUWANIA HATUA YA MAKUNDI LIGI YA MABINGWA

Image
KIKOSI cha Yanga nao wameondoka Alfajiri ya leo kwenda Ethiopia kwa ajili ya mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) ya Ethiopia wakianzia Jumamosi Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, kabla ya kurudiana Uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 20.

SIMBA SC LEO WANALALA UTURUKI MAPEMA KESHO WANAUNGANISHA LIBYA

Image
KIKOSI cha Simba SC kimewasili Istanbul, nchini Uturuki mchana wa leo ambako kitalala kabla ya kuunganisha safari mapema kesho kwenda Tripoli nchini Libya kwa ajili ya mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Kombe la Shirikisho Afrika Ijumaa. Simba itakuwa mgeni wa Al Ahli Septemba 13 Uwanja wa Juni 11 Jijini Tripoli katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Wachezaji waliopo kwenye timu za taifa kwa ajili ya mechi za kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) 2025 wataungana na wenzao Jijini Istanbul usiku wa leo kwa safari ya Tripoli kesho. VIDEO: MENEJA WA SIMBA PATRICK RWEYEMAMU AKIZUNGUMZIA SAFARI 

TABORA UNITED YAICHAPA KAGERA SUGAE 1-0 KWA BAO LA PENALTI

Image
BAO la mkwaju wa penalti la kiungo Mnigeria, Shedrack Asiegbu dakika ya 32 limetosha kuipa Tabora United ushindi wa 1-0 dhidi ya Kagera Sugar katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Shedrack Asiegbu (25) aliyesajiliwa kutoka Rivers United FC ya kwao, Umuabali, Abia - alifunga bao hilo baada ya kiungo Mburkinabe, Yacouba Songné kuangushwa kwenye boksi. Ushindi huo wa pili katika michezo mitatu ya mwanzo wa msimu unaifanya Tabora United ya kocha Mkenya, Francis Kimanzi ifikishe pointi sita baada ya kufungwa 3-0 na Simba Jijini Dar es Salaam kabla ya kushinda 2-1 dhidi ya Namungo huko Ruangwa. Kwa upande wao, Kagera Sugar ya kocha Mganda, Paul Nkata inapoteza mechi ya tatu mfululizo baada ya zile mbili za nyumbani walizofungwa 1-0 na Singida Black Stars na 2-0 mbele ya Yanga.

TAIFA STARS YAANZA RASMI KUWANIA TIKETI YA AFCON 2025

Image
TIMU ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars leo imeweka hai matumaini ya kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) baada ya ushindi wa 2-1 dhidi ya Guinea katika mchezo wao wa pili wa Kundi H Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro nchini Ivory Coast. Haukuwa ushindi mwepesi kwa Taifa Stars, kwani ililazimika kutokea nyuma baada ya mshambuliaji wa Lille ya Ufaransa, Mohamed Lamine Bayo kuanza kuwafungia Guinea dakika ya 57. Lakini nyota wa Azam FC, Feisal Salum Abdallah akaisawazishia Tanzania dakika ya 61, kabla ya kiungo mwenzake, Mudathir Yahya Abbas wa Yanga kufunga bao la ushindi dakika ya 88. Matokeo hayo yanaibakisha Taifa Stars nafasi ya pili ikifikisha pointi nne, nyuma ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) yenye pointi sita, wakati Guinea inaendelea kushika mkia nyuma ya Ethiopia yenye pointi moja. Tanzania ilianza kwa kusuasua kampeni za kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani nchini Morocco baada ya kulazimishwa sare ya bila mabao na Ethiopia

ABUBAKAR, YUSUF BAKHRESA NA FATHER WAWAKABIDHI TIMU MAKOCHA WAPYA

Image
BODI ya Wakurugenzi ya Azam FC ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Abubakar Said Bakhresa leo imetambulisha benchi jipya la Ufundi  kwa wachezaji na wafanyakazi wa timu. Benchi hilo linaundwa na  Kocha Mkuu, Rachid Taoussi, Kocha msaidizi, Badr Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Ouajou Driss na Kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui wote raia wa Morocco. Katika kikao hicho kilichofanyika makao makuu ya klabu, Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam, Abubakar aliambatana na mdogo wake, Yusuf Bakhresa ambaye ndiye Mkurugenzi Mkuu wa klabu na Mwenyekiti wa klabu, Nassor Idrissa 'Father'. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI 

SIMBA SC YAACHANA NA JUMA MGUNDA, MGOSI BOSI TENA QUEENS

Image
KLABU ya Simba imetangaza kuachana na Kocha Juma Ramadhani Mgunda wa timu yake wanawake, Simba Queens na sasa kikosi hicho kitakuwa chini ya Mussa Hassan Mgosi.

AZAM FC SASA BENCHI LA UFUNDI NI LA MOROCCO

Image
KLABU ya Azam FC imetambulisha benchi jipya la Ufundi chini ya Kocha Mkuu Mmoroco, Rachid Taoussi (65) mwenye uzoefu wa kufundisha kuanzia mwaka 1992. Taoussi anajiunga na Azam FC kwa Mkataba wa mwaka mmoja kwa pamoja na wasaidizi wake watatu, Kocha Msaidizi, Ouajou Driss, Kocha wa utimamu wa mwili, Badr Eddine na Kocha wa makipa, Rachid El Mekkaoui wote Wamorocco.  GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI ZA WASAIDIZI WAKE

SERENGETI GIRLS WATWAA UBINGWA UNAF BAADA YA SARE NA TUNISIA

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls imefanikiwa kutwaa ubingwa wa michuano ya Kaskazini mwa Afrika (UNAF) licha ya sare ya bila kufungana na wenyeji, Tunisia leo Uwanja wa Ariana. Serengeti Girls wanatwaa taji hilo kufuatia kumaliza mechi zake tatu bila kupoteza, mbili za awali wakishinda 4-1 dhidi ya Misri na 5-3 dhidi ya Morocco hapo hapo Uwanja wa Ariana. GONGA KUTAZAMA PICHA VIDEO SERENGETI GIRLS WAKISHANGILIA UBINGWA WA UNAFANYA

TAIFA STARS WAWASILI SALAM IVORY COAST KUISUBIRI GUINEA JUMANNE

Image
KIKOSI cha timu ya taifa ya soka ya Tanzania, Taifa Stars kimewasili salama nchini Ivory Coast kwa ajili ya mchezo wao wa pili wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) dhidi ya Guinea Jumanne kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro. Taifa Stars ilianza kwa kusuasua kampeni za kuwania tiketi ya AFCON ya mwakani baada ya kulazimishwa sare ya bila mabao na Ethiopia Jumatano Uwanja w Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa upande wao, Guinea baada ya kichapo cha 1-0 jana kutoka kwa wenyeji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa – wanaanza safari ya kuelekea Yamoussoukro. DRC nao wanasafiri kuja Dar es Salaam kumenyana na Ethiopia Jumatatu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dr es Salaam. Jumla ya nchi 52 zinashiriki hatua ya makundi ya kuwania tiketi ya AFCON 2025, mchuano ulioanza jana na utaendelea hadi Novemba 19 mwaka huu – na washindi wawili wa makundi yote 12 watatengeneza

JKU YAANZA NA MOTO LIGI YA ZENJI, YAITWANGA INTER 3-1 AMAAN

Image
MABINGWA watetezi, JKU wameanza vyema Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar baada ya ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Inter Zanzibar jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanibar. Mabao ya JKU yamefungwa na Koffi Hamza dakika ya saba, Neva Kaboma dakika ya 65 na Tariq Mohammed dakika ya 89, wakati bao pekee la Inter Zanzibar limefungwa na Abdillah Hassan dakika ya 15. Ligi Kuu ya PBZ Zanzibar itaendelea kesho kwa mechi nyingine mbili; Mlandege na Chipukizi Uwanja wa New Amaan Complex na Mwenge dhidi ya KVZ Uwanja wa Gombani, Pemba zote zikianza Saa 10:00 jioni. Jumapili kutakuwa na mechi mbili pia; Mwembe Makumbi na New City New Amaan Complex na Tekeleza dhidi ya Kipanga Uwanja wa Gombani, zote pia zikianza Saa 10:00 jioni. Jumatatu Mafunzo watamenyana na KMKM Uwanja wa Annex A na Uhamiaji dhidi ya Junguni Annex B, wakati Jumanne raundi ya kwanza itakamilishwa kwa mchezo kati ya Malindi na Zimamoto.

MAXI MPIA NZENGELI APIGA ZOTE MBILI YANGA YAICHAPA COSMO 2-0

Image
KIUNGO Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli amefunga mabao yote, Yanga ikiibuka na ushindi wa 2-0 dhidi ya Cosmopolitan Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC),Mwenge Jijini Dar es Salaam.  Huo ni mchezo wa pili dhidi ya timu za Daraja la Kwanza ndani ya siku tatu, baada ya juzi Yanga kuichapa Kiluvya United mabao 3-0 hapo hapo KMC siku hiyo mabao yakifungwa na viungo Shekhan Khamis, Salum Abubakar na mshambuliaji mkongo, Jean Baleke. Mechi kwa Yanga ni sehemu ya maandalizi ya michezo yao ya Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya CBE SA (Commercial Bank of Ethiopia Sports Association) ya Ethiopia wakianzia ugenini Septemba 14 Uwanja wa Abebe Bikila Jijini Addis Ababa, kabla ya kurudiana Uwanja wa Benjamin Mkapa Septemba 20.

AZAM FC YAINGIA MKATABA WA USHIRIKIANO NA KLABU YA AIK YA SWEDEN

Image
KLABU ya imepiga hatua kwa kutanua wigo wake wa kuwa klabu bora nchini na Afrika kwa ujumla baada ya leo kuingia mkataba wa miaka mitano na Klabu ya AIK Football ya Sweden. Mkataba huo utakaodumu hadi mwaka 2029, una lengo la kutoa nafasi kwa wachezaji wa kituo cha kukuzia vipaji cha Azam FC kufanya mazoezi na kuendelezwa katika kituo cha kukuza vipaji cha AIK Football. Kupitia mkataba huo, wachezaji watakaofanya vizuri katika kituo cha kukuzia vipaji cha Azam FC, watapata nafasi ya kwenda Stockholm, Sweden kufanya mazoezi na AIK Football.  Wakiwa Sweden, wachezaji wa Azam FC watapata mafunzo chini ya wataalam waliobobea na wale watakaofanya vizuri watajiunga na kikosi cha kwanza cha timu ya AIK Football bila kusubiri mlolongo mrefu. Makamu Mwenyekiti wa Azam FC, Omary Kuwe amesema mkataba huu unatoa nafasi kwa wachezaji chipukizi wa Azam FC kutimiza ndoto zao za kucheza Ulaya. Kwa upande wake, Ofisa Mtendaji Mkuu wa AIK Football, Fredrik Soderberg amesema amefurahishwa na ushi

SERENGETI GIRLS YAWACHAPA MABINTI WA MOROCCO 5-3 UNAF

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls leo imeendeleza ubabe katika michuano ya Kaskazini mwa Afrika (UNAF) baada ya kuichapa Morocco mabao 5-3 Uwanja wa Ariana Jiji la Pwani, Ariana Kaskazini Mashariki kwa Tunisia. Mabao ya Serengeti Girls yamefungwa na Mwatima Mwarabu mawili, Yasinta Joseph Mitoga moja na Winfrida Gerlad mawili. Huo unakuwa ushindi wa pili kwa Serengeti Girls kutoka ukanda wa CECAFA wakiwa kama waalikwa kwenye michuano hiyo baada ya kuichapa Misri 4-1 katika mchezo wa kwanza Uwanja wa Manispaa wa Kram mjini Kram. Siku hiyo mabao ya Serengeti Girls yalifungwa na Mwatima Mwarabu mawili, Yasinta Joseph Mitoga na Jamila Rajab Mnunduka moja kila mmoja. Katika michuano hiyo inayofikia tamati Septemba 9, Serengeti Girls watarudi Uwanja wa Ariana Jumamosi kuanzia Saa 10:30 jioni kadhalika kumenyana na wenyeji, Tunisia kukamilisha mechi zao.

TAIFA STARS YAAMBULIA SULUHU KWA ETHIOPIA LEO DAR KUFUZU AFCON

Image
TIMU ya soka ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, imeanza kwa sare ya bila mabao na Ethiopia katika mchezo wa kwanza wa Kundi F kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON 2025) usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Suluhu hiyo inamaanisha Taifa Stars wamekosa zawadi ya Sh. Milioni 20, ahadi ya klabu za Azam, Simba na Yanga kama wangeshinda kuanzia mabao matatu na 5 nyingine kutoka kwenye mfuko wa Goli la Mama, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan. Mechi ya pili ya Kundi F itafuatia Ijumaa kwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) kuwa wenyeji wa Guinea kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Martyrs de la Pentecôte Jijini Kinshasa. Mechi za pili za Kundi hilo Ethiopia watakuwa wenyeji wa DRC Septemba 9 hapa hapa Mkapa, wakati Taifa Stars watawafuata Guinea Septemba 10 mechi ambayo itachezwa Uwanja wa Charles Konan Banny de Yamoussoukro mjini Yamoussoukro nchini Ivory Coast. Jumla ya nchi 52 zinatarajiwa kushiriki hatua ya makundi y

KIUNGO WA ZAMANI WA YANGA ABDUL MANENO 'DENIS LAW' AFARIKI DUNIA

Image
Abdul Maneno Kibavu, wa kwanza kulia waliosimama katika kikosi cha Yanga mwaka 1998 KIUNGO wa zamani wa klabu ya Yanga, Abdul Maneno Kibavu 'Denis Law' (54) amefariki dunia jana majira ya Saa 5 usiku katika Hospitali ya Muhimbili alipokuwa amelazwa kwa matibabu ya moyo. Kwa mujibu wa mdogo wa marehemu, Maabad Maneno Kibavu, mchezaji huyo amefariki baada ya kusumbuliwa na maradhi ya Moyo tangu Aprili mwaka huu na matbabu yake yalianza katika Hospitali ya Amana, kabla ya kuhamishiwa Muhimbili, wadi ya Jakaya.  Msiba upo nyumbani kwa marehemu, Mtaa wa Gombero, Magomeni Mwembechai Jijini Dar es Salaam na mwili utaagwa Saa 7 mchana kabla ya safari ya mazishi, kijiji kwao, Yombo, Bagamoyo, Pwani. Abdul Maneno alijiunga na Yanga mwaka 1998 akitokea Sigara ya Dar es Salaam na akacheza hadi mwaka 2000 alipokwenda Msumbiji kumalizia soka yake. Enzi zake Maneno alikuwa anafananishwa na mshambuliaji wa zamani wa Kimataifa wa Scotland, Denis Law aliyetamba Manchester United k

SERENGETI GIRLS YAWACHAPA MISRI 4-1 LEO TUNISIA

Image
TIMU ya taifa ya wasichana chini ya umri wa miaka 17, Serengeti Girls leo imeibuka na ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Mısri katika michuano ya Nchi za Kaskazini mwa Afrika (UNAF) Uwanja wa Manispaa wa Kram mjini Kram nchini Tunisia. Mabao ya Serengeti Girls ambao ni waalikwa kwenye michuano hiyo yamefungwa na Mwatima Mwarabu mawili, Yasinta Joseph Mitoga na Jamila Rajab Mnunduka moja kila mmoja. Katika michuano hiyo inayofikia tamati Septemba 9, Serengeti Girls watarudi uwanjani keshokutwa kumenyana na Morocco, kabla ya kukamilisha kazi kwa kucgeza na wenyeji, Tunisia Jumamosi mechi zote zikipigwa Uwanja wa Ariana kuanzia Saa 10:30 jioni kadhalika.

AZAM FC YAACHANA NA KOCHA DABO BAADA YA MIEZI 15 TANGU AWASILI

Image
KLABU ya Azam FC imeachana na kocha wake Msenegal, Youssoupha Dabo (44) baada ya miezi 15 ya kuwa kazini tangu awasili kutoka ASC Jaraaf ya kwao. Uamuzi huu unafuatia mwanzo mbaya wa msimu kwa Azam FC, ikifungwa 4-1 na Yanga katika Fainali ya Ngao ya Jamii, kabla ya kutolewa na APR katika Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika, ikichapwa 2-0 Kigali baada ya kushinda 1-0 Dar es Salaam. Aidha, Azam FC iliambulia sare ya bila mabao na wenyeji, JKT Tanzania katika mchezo wao wa kwanza Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, matokeo ambayo yalifuatiwa na tetesi na kocha Dabo kuondolewa kazini.

KOCHA WA KABUMBU EDNA LEMA ‘MOURINHO’ AREJEA YANGA PRINCESS

Image
KLABU ya Yanga imemrejesha Kocha Edna Lema ‘Mourinho’ Katika timu ya wanawake, Yanga Princess. Lema alifanya kazi nzuri Yanga Princess kwa misimu miwili, kabla ya kuachana na timu hiyo mwaka juzi na kwenda kuwa Kocha Msadizi wa timu ya wanaume ya Biashara United ya Mara. Lakini baada ya juhudi za kujaribu kuirejesha Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Biashara United kukwama msimu uliopita, Lema ameamua kurejea kufundisha wanawake.

AHOUA MCHEZAJI BORA, FADLU KOCHA BORA LIGI KUU MWEZI AGOSTI

Image
KIUNGO wa Simba SC, Muivory Coast Jean Charles Ahoua (22) ameshinda Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara kwa mwezi Agosti, huku kocha wake, Fadluraghman 'Fadlu' Davids akishinda Tuzo ya Kocha Bora. Kwa pamoja, wawili hao, Fadlu na Ahoua wameisaidia Simba kukusanya pointi sita katika mechi za mwanzo za msimu, wakichapa Tabora United 3-0 na Fountain Gate 4-0 Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Dar es Salaam. Kwa mwezi huo wa kwanza wa msimu, Tuzo ya Ashraf Omar akibeba Tuzo ya Meneja Bora wa Uwanja kwa kazi yake nzuri Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, uliopo Mbweni Jijini Dar es Salaam.