Posts

Showing posts from June, 2024

ENGLAND NA HISPANIA ZATINGA ROBO FAINALI EURO 2024

Image
TIMU za England na Hispania zimefanikiwa kutinga Robo Fainali ya Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ baada ya kuzitoa Slovakia na Georgia jana nchini Ujerumani. Uwanja wa Arena AufSchalke mjini Gelsenkirchen mchezo ulilazimika kwenda hadi 120 baada ya kiungo wa Real Madrid, Jude Victor William Bellingham kuisawazishia England dakika ya 90’+5 na kufuatia mshambuliaji wa  Slavia Prague, Ivan Schranz kuanza kuifungia Slovakia dakika ya 25 na mchezo kuhamia kwenye dakika 30 za nyongeza. Alikuwa Nahodha na mshambuliaji wa Bayern Munich, Harry Edward Kane aliyeifungia England bao la ushindi dakika ya kwanza tu ya dakika za nyongeza na kuipa tiketi ya Robo Fainali ambako itakutana na Uswisi iliyowatoa mabingwa watetezi, Italia juzi. Shughuli ilikuwa nyepesi tu Hispania Uwanja wa RheinEnergieStadion Jijini Cologne, kwani licha ya kutanguliwa kwa bao la kujifunga la beki wa Real Sociedad, Robin Le Normand dakika ya 18, mwishowe ilishinda 4-1. Mabao ya Hispania yalifungwa na viungo,

MWENYEKITI WA ZAMANI YANGA YUSSUF MAJI AFARIKI DUNIA

Image
ALIYEWAHI kuwa Mwenyekiti wa Yanga SC, Yussuf Mehboob Manji amefariki dunia mapema leo nchini Marekani alipkwenda kwa matibabu.

AZAM FC YASAJILI KIUNGO ALIYECHEZA LIGI ZA MISRI, SERBIA NA CZECH

Image
KLABU ya Azam FC imemtambulisha kiungo mshambuliaji, Nassor Saadun Hamoud (23) kuwa mchezaji wake mpya wa sita kuekelea msimu ujao. Taarifa ya Azam FC ambayo msimu ujao pamoja na mashindano ya nyumbani, Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara na Kombe la CRDB Bank pia itashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika - imesem Hamoud amesaini mkataba wa mwaka mmoja wenye kipengele cha kuongeza. Hamoud alizaliwa Machi 23, mwaka 2001 Manispaa ya Temeke Jijini Dar es Salaam na kisoka aliibukia timu ya vijana ya Kagera Sugar, kabla ya kupandishwa timu ya wakubwa mwaka 2017. Mwaka 2018 alikwenda Tersana ya Misri hadi mwaka 2020 akahamia Zarkovo alikocheza hadi kwa nusu msimu akaenda Šumadija Aranđelovac zote za Serbia, kabla ya mwaka  2021 kupelekwa kwa mkopo Vyškov Czech. Hamoud ambaye mwaka 2021 aliitwa timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 20 'Ngorongoro Heroes' - msimu  uliopita alirejea nchini na kujiunga na Geita Gold ambayo imeshuka daraja na sasa anahamishia maisha yake ya soka Chamazi

YANGA SC YASHINDA 4-1 NA KUTWAAA KOMBE LA SAFARI LAGER

Image
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC jana walifanikiwa kutwaa taji la Safari Lager Cup baada  ya ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Kombaini ya Safari Champions katika mchezo wa kirafiki Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam.  Katika mchezo huo ambao Yanga ilitumia wachezaji wake wa timu ya vijana na wachache wa kikkosi cha kwanza akiwemo beki Mkongo, Joyce Lomalisa Mutambala - mabao yake yalifungwa na Omary Mfaume, Shekhan, Prosper na Hussein. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

AZAM FC YARIDHIA PRINCE DUBE KUONDOKA BAADA YA KUKAMILISHA TARATIBU

Image
KLABU ya Azam FC imeridhia kuondoka kwa mshambuliaji wake Mzimbabwe, Prince Mpumelelo Dube (27) kufuatia kukamilisha taratibu za kuvunja mkataba wake. Dube alijiunga na Azam FC Agosti mwaka 2020 akitokea The Highlanders ya kwao, Bulawayo baada ya awali kuzitumikia SuperSport United na Black Leopards kwa vipindi tofauti.

CEO WA YANGA AHITIMU KOZI YA CAF NA KUKABIDHIWA CHETI TANGA

Image
  MKURUGENZI wa Ufundi wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Oscar Milambo akimkabidhi Mtendaji Mkuu wa klabu ya Yanga, Mzambia Andy Mtine Cheti cha kuhitimu Kozi ya Maboresho (Refresher) Diploma B ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) leo kituo cha Ufundi cha TFF, Mnyanjani Jijini Tanga. Baadhi ya wengine walioshiriki Kozi hiyo na kuhitimu ni Kocha wa timu za Vijana za Yanga, Vincent Barnabas, Kocha wa Tabora United, Mserbia Goran Kopunovic na wachezaji wa zamani, Steven Nyenge, Jemedari Said na Athumani Cairo. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

TABORA UNITED, BIASHARA UNITED ZATOZWA MAMILIONI

Image
KLABU za Tabora United na Biashara United zimetozwa Faini kwa makosa mbalimbali ikiwemo vurugu za mashabiki na ukiukaji wa kanuni katika mechi mbili baina yao, nyumbani na ugenini katikati ya mwezi huu. Ikumbukwe Tabora United ilinusurika kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United Juni 16 katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa mwisho wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Matokeo hayo yaliifanya Tabora United iitoe Biashara United kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza Juni 12 Uwanja wa Karume, Musoma mkoani Mara. Biashara United iliingia kwenye mchezo huo ikitokea ligi ya NBC Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza m na Tabora United ilitolewa na JKT Tanzania katika mchujo wa Ligi Kuu. GONGA KUSOMA TAARIFA KAMILI YA BODI

BAKHRESA GROUP | FAHARI YETU EPISODE 1-8

Image
 

AZAM FC YAONGEZA MBRAZIL KWENYE BENCHI LA UFUNDI

Image
KLABU ya Azam FC imemtambulisha Mbrazil, Romulo De Oliveira Freitas (46) kuwa Mtaalamu wake mpya wa Matibabu ya Viungo kwa Wachezaji wake kwa mkataba wa mwaka mmoja. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

NYOTA WA PSG, HAKIMI ATOA MISAADA ZAIDI YA SH. BILIONI 1 TANZANIA

Image
BEKI wa kimataifa wa Morocco anayechezea klabu ya PSG, Archraf Hakimi leo  ametoa msaada wa  vifaa mbalimbali kwa wanafunzi  zaidi ya 400 wenye uhitaji maalum kwenye shule ya Sekondari ya Patandi ya jijini Arusha vyenye gharama ya zaidi ya bilioni moja. Baadhi ya vifaa hivyo ni pamoja na  komputa zaidi ya 50,  samani,  vifaa maalum alama nundu, Mashine za kuchomea taka na kuchemshia maji. Katika hafla hiyo ambayo Waziri wa Maliasili na Utalii Mhe. Angellah Kairuki alikuwa mgeni rasmi ambapo aliwakilishwa na Katibu Mkuu wa Maliasili na Utalii, Dkt. Hassan Abbasi mchezaji huyo ameipongeza  Serikali inayoongozwa na Rais  Samia Suluhu Hassan kwa jitihada  kubwa zinazofanyika katika kutoa huduma za elimu kwa watoto wenye uhitaji maalum. Mchezaji huyo ambaye ni mara yake ya kwanza kutoa misaada kupitia taasisi yake nje ya nchi ya Morocco ameuhakikishia Serikali kuwa ataendelea kushiriki kikamilifu kutoa misaada kwa jamii hapa nchini. Aidha, Hakimi ambaye ameletwa nchini kwa mwaliko ma

SHIME AITA 20 TWIGA STARS YA KUCHEZA NA TUNISIA YANGA PRINCESS HAKUNA HATA MMOJA

Image
KOCHA Bakari Nyundo Shime ameita wachezaji 20 kuunda kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars kwa ajili ya michezo miwili ya kirafiki dhidi ya Tunisia na Botswana mapema mwezi ujao. Katika kikosi hicho kitakachoingia kambini Julai 1 hakuna hata mchezaji mmoja wa Yanga Princess, huku mabingwa Simba Queens wakiwa na wachezaji wawili pekee. JKT Queens imeendelea kuwa klabu yenye wachezaji wengi zaidi Twiga Stars, saba huku wengine wakitoka Alliance Girls, Bunda Queens na Amani Queens mmoja kila timu, wakati wengine ni wanaocheza klabu mbalimbali nje ya Tanzania.

UTURUKI NA GEORGIA NAZO ZAFUZU HATUA YA 16 BORA EURO 2024

Image
TIMU za Uturuki na Georgia zimefanikiwa kufuzu Hatua ya 16 Bora Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ baada ya ushindi katika mechi zao za Kundi F jana dhidi ya Ureno na Czechia nchini Ujerumani. Mabao ya winga wa Napoli ya Italia, Khvicha Kvaratskhelia dakika ya pili na mshambuliaji wa Metz ya Ufaransa, Georges Mikautadze dakika ya 57 kwa penalti yaliipa Georgia ushindi wa 2-0 dhidi ya Ureno ya Cristiano Ronaldo Uwanja wa Arena AufSchalke, mjini Gelsenkirchen. Na mabao ya Uturuki yalifungwa na kiungo wa Inter Milan, Hakan Çalhanoğlu dakika ya 51 na mshambuliaji wa Besiktas, Cenk Tosun dakika ya 90’+4, wakati la Czechia lilifungwa na kiungo wa West Ham United dakika ya 66. Ureno na Uturuki zote zimemaliza na pointi sita na kwa pamoja na zinafuzu Hatua ya 16 Bora kutoka Kundi F, wakati Georgia imefuzu kama miongoni mwa timu nne zilizomaliza nafasi ya tatu na wastani mzuri zaidi wa pointi. Mechi za Kundi E zote zilimalizika kwa sare Slovakia 1-1 na Romania na Ukraine 0-0 na Ubelgi

FIFA YAIRUHUSU YANGA SC KUSAJILI WACHEZAJI WAPYA

Image
SHIRIKISHO la Soka la Kimataifa (FIFA) limeifutia Yanga SC adhabu ya kutosajili mchezaji mpya baada ya kukamilisha malipo ya mshambuliaji wake wa zamani, Mzambia Lazarous Kambole.

UMAKINI DARASANI, STEVE NYENGE KWENYE REFRESHER KOZI YA CAF TANGA

Image
KIUNGO wa zamani wa Kimataifa wa Tanzania, Steven Nyenge akisikiliza kwa makini mafundisho ya Kozi ya Maboresho (Refresher) ya Diploma B ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) yanayoendelea Kituo cha Ufundi cha Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mnyanjani Jijini Tanga. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

MZAMIRU YASSIN AONGEZA MKATABA MPYA SIMBA SC HADI MWAKA 2026

Image
KIUNGO Mzamiru Yassin Selemba (28) amesaini mkataba wa mpya wa miaka miwili kuendelea na kazi Simba SC hadi mwaka 2026. Rasmi, Mzamiru anakuwa mchezaji wa kwanza kutajwa kuongeza mkataba Simba SC baada ya wengine sita kuachwa na kusajili mpya mmoja. Walioachwa ni mabeki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda. Aidha, tayari Simba SC imemtambulisha mchezaji mmoja tu mpya, beki chipukizi wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga. KIUNGO Mzamiru Yassin Selemba (28) amesaini mkataba wa mpya wa miaka miwili kuendelea na kazi Simba SC hadi mwaka 2026. Rasmi, Mzamiru anakuwa mchezaji wa kwanza kutajwa kuongeza mkataba Simba SC baada ya wengine sita kuachwa na kusajili mpya mmoja. Walioachwa ni mabeki Mkongo, Henock Inonga Baka ‘Varane’, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumb

ITALIA YAIPOKONYA TONGE MDOMONI DAKIKA YA MWISHO EURO 2024

Image
MABINGWA watetezi, italia wamefanikiwa kutinga hatua ya 16 Bora Kombe la Mataifa Ulaya 'Euro 2024' licha ya sare ya 1-1 na Croatia katika mchezo wa Kundi B usiku wa jana Uwanja wa Leipzig Jijini Leipzig nchini Ujerumani. Kiungo mkongwe wa umri wa miaka 38, Luka Modrić wa Real Madrid alianza kuifungia Croatia dakika ya 55, dakika moja tu tangu mkwaju wake wa penalti uokolewe na kipa Gianluigi Donnarumma. Lakini mashabiki wa Croatia wakifurahia na kuamini wamesonga mbele, kiungo wa Lazio, Mattia Zaccagni aliwainua mashabiki wa Italia na kuwanyamazisha wapinzani kwa kufunga bao la kusawazisha dakika ya nane na mwisho muda wa nyongeza baada ya kutima dakika 90 za kawaida za mchezo. Mechi nyingine ya Kundi B jana bao pekee la mshambuliaji wa Barcelona, Ferran Torres García dakika ya 13 liliipa Hispania ushindi wa 1-0 dhidi ya Albania Uwanja wa Dusseldorf Arena Jijini Dusseldorf. Hispania imeongoza Kundi B kwa pointi zake tisa ikifuatiwa na Italia pointi nne na zote zimefuzu 1

SIMBA SC YATANGAZA RASMI KUACHANA NA HENOCK INONGA BAKA ‘VARANE’

Image
KLABU ya Simba imeachana na beki wa Kimataifa was Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), Henock Inonga Baka ‘Varane’ baada ya kuwatumikia Wekundu wa Msimbazi tangu mwaka 2021 alipowasili kutoka DC Motema Pembe ya kwao, Kinshasa.  Huyo anakuwa mchezaji wa sita kutemwa Simba baada ya beki mwingine wa katı, Kennedy Wilson Juma, viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda. Tayari Simba SC imemtambulisha mchezaji mmoja tu mpya, beki chipukizi wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga.

MBWANA MAKATTA KOCHA MPYA WA TANZANIA PRISONS

Image
KLABU ya Tanzania Prisons imemtambulisha Mbwana Makatta kuwa Kocha wake mpya Mkuu kuelekea msimu ujao wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Makatta mwenye uzoefu wa kufundisha timu mbalimbali za Ligi Kuu kwa zaidi ya miaka 30 - anajiunga na Tanzania Prisons baada ya kuondolewa Pamba Jiji FC kufuatia kuipandisha Ligi Kuu.

ACHRAF HAKİMİ WA PSG MGENI WA RAIS WA YANGA SC

Image
RAIS wa Yanga SC, Hersi Said akiwa na mgeni wake, beki wa Mmorocco mzaliwa wa Hispania, Achraf Hakimi Mouh anayechezea klabu ya  Paris Saint-Germain ya Ufaransa baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege was Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA). Hakimi ameambatana na rafiki zake saba ambao kwa pamoja watakuwa nchini kwa wiki moja na mwenyeji wao, Hersi ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Klabu Afrika (ACA) kutembelea vivutio mbali mbali vya kiutalii nchini. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

KIKOSI CHA MZIZIMA UNITED 1965 ENZI ZA TAIFA CUP

Image
KIKOSI cha timu ya soka ya Kombaini ya Mkoa wa Dar es Salaam ‘Mzizima United’ kabla ya moja ya mechi zake za Kombe la Taifa mwaka 1965, michuano ambayo awali ilikuwa inajulikana kama Sunlight Cup. Kutoka kulia waliosimama ni; marehemu Athuman Kilambo (Yanga), marehemu Mussa Libabu (Sunderland/Simba), Mustafa Choteka (Sunderland/Simba), marehemu Abdulrahman Lukongo (Yanga/Cosmo) Gilbert Mahinya (Sunderland/Simba/Yanga), marehemu Ally Kajo (Sunderland/Simba). Waliochuchumaa kutoka kulia ni Hamisi Kilomoni (Sunderland/Simba), marehemu Badi Saleh (Yanga), marehemu Mohammed Msomali (Yanga/Cosmo), marehemu Maulid Dilunga (Yanga), marehemu Mbaraka Salum Magembe (Sunderland/Simba), Kitwana Manara (Cosmo/Yanga) na marehemu Abdallah Aziz (JWTZ).

UJERUMANI YAMALIZA MECHI ZA KUNDI LAKE KWA SARE

Image
WENYEJ, Ujerumani wamekamilisha mechi zao za Kundi A kwa sare ya kufungana bao 1-1 na Uswisi usiku wa Jumapili Uwanja wa Frankfurt Arena Jijini Frankfurt. Mshambuliaji wa Bologna, Dan Assane Ndoye mwenye asili ya Senegal alianza kuifungia Uswisi dakika ya 28, kabla ya mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Niclas Füllkrug kuisawazishia Ujerumani dakika ya  90’+2. Ujerumani imemaliza na pointi saba kileleni ikifuatiwa na Uswisi pointi tano na zote zinafuzu Hatua ya 16 Bora, wakati Hungary iliyoifunga Scotland 1-0 jana bao la Kevin Csoboth dakika ya 90+10' ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi tatu. Hungary inaweza kwenda Hatua ya 16 Bora kupitia Kapu la washindi wa pili bora, wakati Scotland safari yao imeisha hapa.

SIMBA SC KUWEKA KAMBI MISRI KUJIANDAA NA MSIMU MPYA

Image
KIKOSI cha Simba kinatarajiwa kuondoka nchini mapema Julai kwenda kuweka kambi katika Jiji la Ismailia nchini Misri kujiandaa na msimu mpya wa Ligi Kuu na Kombe la Shirikisho Afrika. VIDEO: AHMED ALLY – AFISA HABARI SIMBA AKIZUNGUMZA 

AZAM FC YAACHA WACHEZAJI WANNE ‘KWA MPIGO’ WAMO WAGENI WAWILI

Image
KLABU ya Azam FC imeachana na wachezaji wake wanne ambao ni mabeki Msenegal, Malickou Ndoye, Edward Charles Manyama na viungo, Ayoub Reuben Lyanga na Mnigeria Isah Aliyu Ndala. Hao wanafanya idadi ya wachezaji walioachwa rasmi kufuatia kumalizika kwa msimu kufika watano baada ya awali kutangaza na beki Mghana, Daniel Amoah. Tayari Azam FC imesajili wachezaji watano wapya ambao ni mshambuliaji Adam Omary Adam kutoka Mashujaa ya Kigoma, beki wa kati, Yoro Mamadou Diaby kutoka Stade Malien alipokuwa anacheza kwa mkopo kutoka akademi ya Yeleen Olympique ya Mali na kiungo mshambuliaji, Muivory Coast, Franck Tiesse kutoka Stade Malien. Wengine ni Wacolombia, kiungo Ever Meza kutoka Leonnes ya kwao na mshambuliaji Jhonier Blanco kutoka Aguilas Doradas ya kwao pia, Colombia. GONGA KUTAZAMA PICHA ZA WACHEZAJI WALIOACHWA AZAM 

DK. TANDAU AZUNGUMZIA USHIRIKI WA TANZANIA OLIMPIKI YA PARIS 2024

Image
MAKAMU wa Rais wa Kamati ya Olimpiki Tanzania (TOC), Dk. Henry Tandau amesema ana matumaini ya Wanariadha wa Tanzania kufanya vyema kwenye Michezo ya Olimpiki inayotarajiwa kufanyika mwezi ujao Jijini Paris nchini Ufaransa.

CLARA LUVANGA: NILIUMIA KUSHUTUMIWA MIMI MWANAUME

Image
MSHAMBULIAJI wa kike wa kimataifa wa Tanzania, Clara Cleitus Luvanga (19) anayechezea klabu ya Al Nassr ya Ligi Kuu ya Wanawake Saudi Arabia amesema aliumia sana kushutumiwa yeye ni mwanaume kiasi ilimuathiri Kisaikolojia na kushindwa kabisa kucheza wakati huo hadi akaondolewa timu ya taifa ya taifa.

TEAM JOB 'WAIFINYANGA FINYANGA' TEAM KIBWANA MECHI YA HISANI MOROGORO,

Image
MECHI ya kirafiki ya Hisani baina ya mebeki wa Yanga, Kibwana Shomari dhidiya Dickson Job na rafiki zao imemalizika kwa Team Job kuibuka na ushindi wa mabao 6-2 dhidi ya Team Kibwana jioni ya leo Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.    Mabao ya Team Job yamefungwa na Hersi Said dakika ya 13, Mzimbabwe Prince Dube dakika ya 27, George Mpole dakika ya 78, Samson Mbangula dakika ya 79 na Edwin Balua dakika ya 90'+4, wakati mabao ya Team Kibwana yote yamefungwa na Simon Msuva dakika ya 30 na 47.  

UHOLANZI NA UFARANSA ZATOSHANA NGUVU, AUSTRIA NA UKRAINE ZASHINDA

Image
TIMU za Uholanzi na Ufaransa jana zimegawana pointi baada ya sare ya bila mabao katika mchezo wa Kundi D Kombe la Mataifa ya Ulaya 'Euro 2024' Uwanja wa Leipzig Jijini Leipzig nchini Ujerumani. Safu ya ushambuliaji ya Ufaransa ilionekana kabisa kupoteza makali yake kutokana na kumkosa Nahodha wake, Kylian Mbappé Lottin aliyeumia pua kwenye mchezo wa kwanza dhidi ya Austria Uwanja wa Merkur Spiel-Arena Jijini Düsseldorf. Katika mchezo huo ambao Ufaransa ilishinda 1-0, Mbappe aliyejiunga na Real Madrid mwezi huu - aliumia pua baada ya kugongana na beki wa Lens ya Ufaransa, Kevin Danso na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji wa AÇ Milan, Olivier Giroud dakika ya 90. Mechi nyingine ya Kundi D jana Austria iliibuka na ushindi wa 3-1 dhidi ya Poland Uwanja wa  Olympia Jijini Berlin.  Sasa msimamo wa Kundi D ni Uholanzi na Ufaransa pointi nne kila moja, zikifuatiwa na  Austria yenye pointi tatu na Poland inayoshika mkia ambayo haina pointi. Mab

CSKA MOSCOW WATUA YANGA KWA ZOEZI MAALUM

Image
  KLABU ya Yanga leo imepokea ugeni wa Maafisa wa klabu ya CSKA Moscow ya Urusi ambao wamekuja kuendesha programu maalumu ya kutambua vipaji vya wanasoka chipukizi nchini. Programu hii itaendeshwa na CSKA Moscow kwa kushirikiana na Young Africans Sports Club, itaanza kesho na itafanyika Dar Es Salaam, Tanga na Zanzibar. Baada ya kuwasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA), Maafisa hao walikutana na uongozi wa Yanga chini ya Rais, Hersi Ally Said. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI

SIMBA SC YATAMBULISHA MKALI MPYA WA KWANZA, NI LAWI WA COASTAL

Image
KLABU ya Simba SC imemtambulisha beki wa katı, Lameck Elias Lawi (18) kutoka Coastal Union ya Tanga kuwa mchezaji wake wa kwanza mpya kuelekea msimu ujao. Na hiyo inafuatia kuacha wachezaji watano akiwemo beki wa katı, Kennedy Wilson Juma Ambasa (29) aliyedumu kikosini tangu Julai 2019 alipowasili kutoka Singida United. Wengine walioachwa Simba SC ni viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.

KENNEDY JUMA NAYE APEWA MKONO WA KWAHERI SIMBA SC

Image
KLABU ya Simba SC imeendelea kuutambulisha Wachezaji inayoachana nao baada ya msimu na safari hii ni beki wa katı, Kennedy Wilson Juma Ambasa  aliyedumu kikosini tangu Julai 2019 alipowasili kutoka Singida United. Kennedy Wilson Juma Ambasa (29) anakuwa mchezaji wa tano kupewa mkono wa kwaheri Simba SC baada ya viungo, Mrundi Saido Ntibanzokiza, Luis Jose Miquissone wa Msumbiji na washambuliaji John Raphael Bocco na Shaaban Iddi Chilunda.

AZAM FC YAACHANA NA BEKİ MGHANA DANIEL AMOAH

Image
KLABU ya Azam FC imeachana na beki wake Mghana, Daniel Amoah (26) baada ya kuitumikia klabu kwa miaka nane tangu alipowasili kutoka Medeama SC ya kwao mwaka 2017.

PAMBA YAVUNJA BENCHI NA TIMU NZIMA, KOPUNOVIC KUUNDA KIKOSI KIPYA

Image
TIMU ya Pamba Jiji FC imevunja benchi zima la Ufundi chini ya kocha mzawa aliyewapandisha Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara, Mbwana Makatta na kumuajiri Mserbia, Goran Kopunovic. Sambamba na kuvunja benchi la Ufundi, Pamba Jiji FC pia imeachana na wachezaji wote waliopandisha timu na kumpa jukumu Goran Kopunović, kocha wa zamani wa Simba SC na Tabora United kuunda kikosi kipya cha Ligi Kuu.

MIQUISSONE NAYE KAFUPISHIWA MWENDO MSIMBAZI

Image
KİUNGO wa Kimataifa wa Msumbiji, Luis Jose Miquissone amekuwa mchezaji wa nne kuachwa Simba SC baada ya kiungo mwenzake, Mrundi Saido Ntibanzokiza na washambuliaji, Shaaban Iddi Chilunda na John Raphael Bocco.

SHAABAN CHILUNDA NAYE AONYESHWA GETI LA KUTOKEA SIMBA SC

Image
MSHAMBULIAJI Shaaban Iddi Chilunda amekuwa mchezaji wa tatu kuachwa na klabu ya Simba SC baada ya kumalizika msimu ikishika nafasi ya tatu kwenye Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara. Chilunda (25) alijiunga na Simba SC mwanzoni mwa msimu akitokea Azam FC, lakini wakati wa dirisha dogo akatolewa kwa mkopo KMC. Anakuwa mchezaji wa tatu kuachwa baada ya aliyekuwa Nahodha John Raphael Bocco na kiungo Mrundi, Saido Ntibanzokiza.

MAREHEMU YOMBAYOMBA: BONDIA PEKEE ALIYELETA MEDALI YA DHAHABU JUMUIYA YA MADOLA

Image
 

URENO NA UTURUKI ZAANZA NA USHINDI PIA EURO 2024

Image
TIMU ya Taifa ya Ureno imeanza vyema Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2020’ baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Jamhuri ya Czech katika mchezo wa Kundi F usiku wa jana Uwanja wa Red Bull Arena Jijini Leipzig nchini Ujerumani. Haukuwa ushindi mwepesi kwa Ureno kwani ililazimika kutoka nyuma baada ya winga wa Slavia Prague, Lukáš Provod kuanza kuifungia Jamhuri ya Czech dakika ya 62 na ndipo beki wa Viktoria Plzeň, Robin Hranáč akajifunga dakika ya 69 kuipatia ‘A Seleção das Quinas’ bao la kusawazisha, kabla ya winga wa Porto, Francisco Fernandes da Conceição kuifungia timu yake bak la ushindi dakika ya 90’+2. Mechi iliyotangulia ya Kundi F Uturuki waliichapa  Georgia 3-1 Uwanja wa Westfalenstadion Jijini Dortmund. Mabao ya Uturuki yalifungwa na beki wa Fenerbahçe, Mert Müldür dakika ya 25, winga wa Real Madrid, Arda Güler dakika ya 65 na kiungo mshambuliaji wa Galatasaray, Muhammed Kerem Aktürkoğlu  dakika ya 90’+7, wakati bao pekee la Georgia lilifungwa na mshambuliaji wa Metz

MTAALAMU SAIDO NTIBANZOKIZA AHITIMISHA UTUMISHI WAKE SIMBA SC

Image
KIUNGO wa Kimataifa wa Burundi, Saido Ntibanzikoza (40) amekuwa mchezaji wa pili kuachwa Simba SC baada ya msimu mmoja na nusu wa kuitumikia timu kwa mafanikio. Ntibanzokiza alijiunga na Simba Januari mwaka jana akitokea Geita Gold kwa misimu yote miwili amekuwa mfungaji bora wa timu. Mchezaji wa kwanza kuachwa Simba ni Nahodha wa timu kwa mafanikio kwa misimu kadhaa, John Raphael Bocco (34) aliyejiunga na timu hiyo mwaka 2017 akitokea Azam FC.

NIGERIA, ZAMBIA NA KENYA KUIWAKILISHA AFRIKA KOMBE LA DUNIA WASICHANA U17

Image
TIMU za Kenya, Zambia na Nigeria ndizo nchi tatu za Afrika zitakazoiwakilisha Afrika kwenye michuano ya nane ya Kombe la Dunia la FIFA kwa wasichana chini ya umri wa miaka 17 inayotarajiwa kufanyika kuanzia Oktoba 16 hadi Novemba 3 mwaka huu Jamhuri ya Dominica. Nigeria itakwenda kwenye Fainali hizo kwa mara ya sita ikiwa timu pendwa zaidi Afrika, huku Zambia ikipewa heshima pia kwa kiwango chao kizuri katika michuano iliyopita, wakati kwa Kenya wanakwenda kushiriki fainali hizo kwa mara ya kwanza. Flamingos ya Nigeria ilikata tiketi yake baada ya kuitoa Liberia kwa jumla ya mabao 6-1, wakishinda 4-1 ugenini na 2-0 nyumbani, Abuja, wakati Zambia Copper Princesses wa Zambia imefuzu kwa kuitoa Morocco kwa jumla ya 3-1, ushindi walioupata nyumbani baada ya sare ya bila mabao Morocco na Kenya, Harambee Starlets waliitoa Burundi jijini Nairobi kwa jumla ya mabao 5-0. Fainali za Kombe la Dunia la FIFA U17 2024 zitashirikisha timu tatu za Afrika pamoja na England, Brazil, Colombia, Ecua

UFARANSA YASHINDA LAKINI MBAPPE AUMIA PUA NA KUTOLEWA NJE

Image
UFARANSA imeanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Austria katika mchezo wa Kundi D usiku wa Jumatatu Uwanja wa Merkur Spiel-Arena Jijini Düsseldorf nchini Ujerumani. Lilikuwa bao la kujifunga la beki wa kushoto wa Leeds United, Maximilian Wober dakika ya 38  lililoipa mwanzo mzuri Les Bleus na mbaya Austria katika Fainali za Euro 2024. Hata hivyo, Ufaransa ilipata pigo baada ya Nahodha wake, Kylian Mbappe kuumia pua kufuatia kugongana na beki wa Lens ya Ufaransa, Kevin Danso na kushindwa kuendelea na mchezo nafasi yake ikichukuliwa na mshambuliaji wa AÇ Milan, Olivier Giroud dakika ya 90. Katika mechi zilizotangulia za Kundi E, Romania iliichapa Ukraine 3-0, mabao ya viungo Nicolae Stanciu dakika ya 29, Răzvan Marin dakika ya 53 na mshambuliaji Denis Drăguș dakika ya 57 Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich, wakati Slovakia iliilaza Ubelgiji 1-0 bao la mshambuliaji Ivan Schranz dakika ya sana Uwanja wa Waldstadion Jijini Frankfurt.

BOCCO MCHEZAJI WA KWANZA KUPEWA ‘THANK YOU’ SIMBA SC

Image
MSHAMBULIAJI na aliyekuwa Nahodha wa timu kwa mafanikio kwa misimu kadhaa, John Raphael Bocco amekuwa mchezaji wa kwanza kuachwa Simba SC. Bocco (34) aliyejiunga na Simba SC mwaka 2017 akitokea Azam FC alicheza nusu ya kwanza tu ya msimu uliomalizika, kabla ya kuumia kwenye michuano ya Kombe la Mapinduzi visiwani Zanzibar.  Alilikuwa sehemu ya wachezaji wa akiba kwenye mechi ya kwanza ya Mapinduzi dhidi ya JKU Januari 1 mwaka huu Simba SC ikishinda 3-1 na akapangwa aanze mechi ya pili, bahati mbaya akaumia katika mazoezi ya kupasha misuli moto Januari 3 dhidi ya Singida Fountain Gate na ndio akamaliza msimu. Simba ilishinda 2-0 mechi hiyo ya Kundi B na kwenda Robo Fainali na wakafika hadi Fainali wakafungwa 1-0 na Mlandege Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Tangu aumie Bocco amepewa jukumu la kufundisha kikosi cha timu ya vijana cha Simba chini ya umri wa miaka 17.

ENGLAND NA UHOLANZI ZAANZA VYEMA EURO 2024

Image
TIMU ya England imeanza vyema Kombe la Mataifa ya Ulaya ‘Euro 2024’ baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Serbia usiku wa jana katika mchezo wa Kundi C Uwanja wa AufSchalke, Gelsenkirchen nchini Ujerumani. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo wa Real Madrid, Jude Victor William Bellingham dakika ya 13 kwa kichwa baada ya krosi nzuri kutoka upande wa kulia. Mechi nyingine ya Kundi C jana  Slovenia ilitoka sare ya 1-1 na Denmark Uwanja wa MHPArena, Jijini Stuttgart . Kiungo wa Manchester United, Christian Dannemann Eriksen  alianza kuifungia Denmark dakika ya 17, kabla ya beki wa kishoto wa Górnik Zabrze ya Poland, Erik Janža kuisawazishia Slovenia dakika ya 77. Mechi moja ya Kundi D ilipigwa pia jana Uholanzi ikiibuka na ushindi wa 2-1 dhidi ya Poland Uwanja wa Volksparkstadion Jijini Hamburg. Mabao ya Uholanzi yalifungwa na winga wa Liverpool, Cody Mathès Gakpo dakika ya 29 na mshambuliaji wa Burnley, Wout François Maria Weghorst dakika ya 83 baada ya mshambuliaji wa Antal

NYOTA WA ANGOLA AINUSURU TABORA UNITED KUSHUKA DARAJA

Image
TIMU ya Tabora United imenusurika kushuka daraja baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Biashara United katika mchezo wa marudiano wa mchujo wa mwisho wa kuwania kubaki Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Ali Hassan Mwinyi mjini Tabora. Shujaa wa Tabora United ni mshambuliaji wa Kimataifa wa Angola, Patrick Lembo Aufumu aliyefunga mabao yote mawili, la kwanza kwa penaltı dakika ya 27 na la pili dakika ya 55 akimalizia mpira wa adhabu. Kwa matokeo hayo, Tabora United inaitoa Biashara United kwa ushindi wa jumla wa 2-1 kufuatia kufungwa 1-0 kwenye mchezo wa kwanza katikati ya wiki. Ikumbukwe Biashara United imetoka ligi ya NBC Championship ambako iliitoa Mbeya Kwanza katika mchezo na Tabora United ilitolewa na JKT Tanzania katika mchezo wa Ligi Kuu.

WENYEJI UJERUMANI WAANZA KWA KISHINDO EURO 2024, YASHINDA 5-1

Image
WENYEJI, Ujerumani jana wameanza vyema Fainali za Kombe la Mataifa ya Ulaya 'Euro 2024' baada ya kuichapa Scotland mabao 5-1 katika mchezo wa Kundi A Uwanja wa Allianz Arena Jijini Munich. Mabao ya 'Die Mannschaft' jana yalifungwa na kiungo wa Bayer Leverkusen, Florian Richard Wirtz dakika ya 10, mshambuliaji wa Bayern Munich, Jamal Musiala dakika ya 19 na kiungo wa Arsenal, Kai Lukas Havertz kwa penalti dakika ya 45'+1. Mabao mengine yalifungwa na mshambuliaji wa Borussia Dortmund, Niclas Fullkrug dakika ya 68 na kiungo wa Borussia Dortmund, Emre Can dakika ya 90'+3, wakati bao pekee la ' The Tartan Army' alijifunga beki wa Real Madrid,  Antonio Rüdiger dakika ya 87. Mechi nyingine ya Kundi A leo, Uswisi imeifunga Hungary mabao 3-1 Uwanja wa RheinEnergie Jijini Cologne. Mabao yake yakifungwa na mshambuliaji mwenye asili ya Ghana, Kwadwo Antwi Duah dakika ya 12, kiungo Michel Aebischer dakika ya 45 na mshambuliaji mwenye asili ya Cameroon, Breel D

USAJILI MSIMU MPYA DIRISHA WAZI KUANZIA KESHO

Image
DIRISHA la usajili msimu mpya wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2024-25 na madaraja ya chini pamoja na Ligi za Wanawake litafunguliwa rasmi kesho. Mshambuliaji Mzimbabwe ambaye ameondoka Azam FC anahusishwa na vigogo wote wawili, Simba na Yanga - je, ataubukia wapi?

SERIKALI YAWAPA TAIFA STARS MILIONI 110 KUIFUNGA ZAMBIA KWAO

Image
WAZIRI wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk. Damas Daniel Ndumbaro leo amekabidhi Shilingi Milioni 110 kwa timu ya soka ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, yote ikiwa zawadi kutoka kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan. Waziri Ndumbaro amekabidhi mfano wa Hundi ya Sh. Milioni ambazo Rais Samia aliahidi iwapo Taifa Stars itaifunga Zambia na Fedha taslimu Sh. Milioni ambayo Mheshimiwa Rais hutoa kwa kila bao linalofungwa timu ya Taifa. Ikumbukwe juzi Taifa Stars iliibuka na ushindi wa 1-0 dhidi ya wenyeji, Zambia katika mchezo wa Kundi E kufuzu Kombe la Dunia 2026 uliofanyika Uwanja wa Levy Mwanawasa Jijini Ndola. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee mshambuliaji wa KMC, Waziri Junior Shentembo dakika ya tano akimalizia pası ya kiungo wa Yanga SC, Mudathir Yahya Abbas. Kwa ushindi huo, Taifa Stars imefikisha pointi sita katika mchezo wa tatu na kusogea nafasi ya pili nyuma ya vinara, Morocco ‘Simba wa Atlasi’ ambao wamecheza mechi mbili, wakati Zambia