Posts
Showing posts from August, 2024
ATEBA AFUNGUA AKAUNTI YA MABAO SIMBA YATOA SARE NA EL HILAL
- Get link
- X
- Other Apps
KLABU ya Simba imetoa sare ya kufungana bao 1-1 na Al Hilal Omdurman ya Sudan katika mchezo wa kirafiki uliofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam jioni ya leo. Mshambuliaji mpya, Mcameroon Christian Leonel Ateba Mbida (25) alianza kuifungia Simba katika mechi yake ya kwanza tangu asajiliwe kutoka USM Alger ya Algeria dakika ya 25, kabla ya winga wa kushoto Muivory Coast, N'guessan Serge Archange Pokou kuisawazishia Hilal dakika ya 76. Mchezo huo ulikuwa wa matayawisho kwa timu zote kujiandaa na mechi za Raundi ya Kwanza za michuano ya Afrika, A Hilal wakicheza Ligi ya Mabingwa na Simba Kombe la Shirikisho Afrika. Simba itakuwa mgeni wa Al Ahli Septemba 13 Uwanja wa Juni 11 Jijini Tripoli katika mchezo wa kwanza Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika, kabla ya timu hizo kurudiana Septemba 20 Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Kwa upande wao, Al Hilal watakuwa wageni wa San-Pédro FC Septemba 13 Uwanja wa Laurent Pok
FOUNTAIN GATE YAICHAPA NAMUNGO FC 2-0 PALE PALE RUANGWA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Fountain Gate imeibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Fountain Gate yamefungwa na Edgar William dakika ya 30 na Suleiman Mwalimu dakika ya 45’+3 huo ukiwa ushindi wa kwanza katika mechi mbili za mwanzo za simu, zote wakicheza ugenini wakitoka kuchapwa 4-0 na Simba Jijini Dar es Salaam Jumapili. Kwa Namungo FC leo wamepoteza mechi ya pili mfululizo nyumbani baada ya kuchapwa 2-1 na Tabora United katika mchezo wa kwanza.
KMC YAAMBULIA SARE KWA COASTAL UNION, 1-1 MWENGE
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, KMC wamelazimishwa sare ya kufungana bao 1-1 na Coastal Union katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC), MWENGE Jijini Dar es Salaam. Katika mchezo huo wa kwanza wa msimu kwa timu zote, KMC walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa kiungo wa Kimataifa wa Somalia, Ibrahim Elias dakika ya 32, kabla ya mshambuliaji Maabad Maulid kuisawazishia Coastal Union dakika ya 85 kwa penaltı.
JKT TANZANIA NA AZAM FC HAKUNA MBABE, SARE 0-0 MBWENI
- Get link
- X
- Other Apps
SIMBA QUEENS YATUPWA NJE LİGİ YA MABINGWA AFRİKA CECAFA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Simba Queens imetupwa nje ya kinyang’anyiro cha tiketi ya Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-2 na Polisi Bullets ya Kenya leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mabao ya Polisi yamefungwa na Lucy Kwekwe dakika ya 29, Diana Wacera dakika ya 60 na Rebecca Okwaro dakika ya 82, wakati ya Simba Queens yote yamefungwa na kiungo Mkenya, Vivian Corazone Aquino Odhiambo. Sasa Polisi itamenyana na wenyeji, CBE katika Fainali Jumatano, ambao wameitoa Kawempe Muslim ya Uganda kwa kuichapa mabao 2-1 leo pia. Simba Queens itawania nafasi ya tatu dhidi ya Kawempe katika mchezo wa utangulizi Jumatano.
DICKSON JOB AREJESHWA TAIFA STARS MECHI ZA KUFUZU AFCON
- Get link
- X
- Other Apps
BEKİ wa Yanga, Dickson Nickson Job amerejeshwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania Taifa, Taifa Stars kwa ajili ya Michezo miwili ya Kundi H Kufuzu Fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON) dhidi ya Ethiopia na Guinea mapema mwezi ujao. Job aliwekwa kando Taifa Stars baada ya kukaidi agizo la Kocha Hemed Suleiman Morocco kucheza beki ya pembeni, lakini baada ya kuomba radhi sasa amerejeshwa. Taifa Stars itakuwa mwenyeji wa Ethiopia Septemba 6, kabla ya kusafiri kuwafuata Guinea ambao watachezea nchini Ivory Coast. Timu nyingine katika Kundi hilo kuwania tiketi ya AFCON ya 2025 itakayofanyika nchini Morocco ni DRC na ambayo itacheza na Taifa Stars Okoba 14 Jjjini Dar es Salaam.
MAKAMBO, DJUMA SHABANI WAFUNGA PENALTI TABORA UNITED YAICHAPA NAMUNGO 2-1
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Tabora United imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya wenyeji, Namungo FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Majaliwa, Ruangwa mkoani Lindi. Mabao ya Tabora United yamefungwa na mshambuliaji Mkongo, Heritier Ma Olongi Makambo dakika 72 kwa penalti na beki mzawa, Salum Abdallah Chuku dakika ya 90'+2, wakati bao pekee la Namungo FC limefungwa na beki Mkongo, Djuma Shabani kwa penalti pia dakika ya 60. Ni ushindi wa kwanza katika mchezo wa pili ikitoka kufungwa 3-0 na Simba wiki iliyopita Dar es Salaam, wakati Namungo FC leo imecheza mechi yake ya kwanza ya msimu.
COASTAL UNION YAUMALIZA MWENDO KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA MAPEMA TU
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Coastal Union imetupwa nje ya michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya sare ya kufungana na Bravos do Maquis ya Angola leo katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Wagosi wa Kaya au Wana Mangush kwa majina ya utani wanatupwa nje kufuatia kuchapwa 3-0 na Bravos do Maquis katika mchezo wa kwanza Jumamosi ya wiki iliyopita Uwanja wa Taifa wa Tundavala mjini Lubango nchini Angola. Bravos do Maquis sasa itakutana na St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) katika Hatua ya 32 Bora kuwania kuingia Hatua ya 16 Bora, inayochezwa kwa mtindo wa makundi. Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Simba SC wataanzia Raundi ya Kwanza kwa kumenyana na Al Ahli Tripoli ya Libya iliyoitoa Uhamiaji ya Zanzibar.
SIMBA SC YAIRARUA FOUNTAIN GATE 4-0 LEO KINONDONI
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Simba imeibuka na ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Fountain Gate katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni (KMC) Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Simba SC yamefungwa na kiungo mzawa, Edwin Charles Balua dakika ya 13, mshambuliaji Mganda, Steven Dese Mukwala dakika ya 44, kiungo Muivory Coast, Jean Charles Ahoua dakika ya 58 na mshambuliaji mzawa, Valentino Mashaka Kusengama dakika ya 81. Ushindi huo wa pili katika mchezo wa pili tu wa msimu unaifanya Simba ifikishe pointi sita na kupanda kileleni ikiizidi wastani wa mabao Singida Black Stars, wakati kwa Fountain Gate leo ilikuwa mechi yao ya kwanza.
YANGA SC YAICHAPA VITAL'O 6-0, KUCHEZA NA WAHABESHI KUWANIA MAKUNDI
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA wa mataji yote Tanzania, Yanga SC wamefanikiwa kufuzu Hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Vital’O ya Burundi katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na kiungo Muivory Coast, Peodoh Pacome Zouzoua dakika ya 14 kwa penalti, mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 49, kiungo Mzambia Clatous Chota Chama dakika ya 51, mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo na viungo, Mburkinabe Stephane Aziz Ki dakika ya 78 na Mudathir Yahya Abbas dakika ya 86. Yanga inasonga mbele kwa ushindi wa jumla wa 10-0, kufuatia kuichapa Vital'O 4-0 kwenye mchezo wa kwanza hapo hapo Azam Complex Jumamosi iliyopita, mabao ya Dube dakika ya sita, Chama dakika ya 68, dakika ya 74 na Aziz Ki kwa penalti dakika ya 90'+1. Sasa Yanga itakutana na CBE (Benki ya Biashara Ethiopia) ambayo imeitoa SC Villa ya Uganda kwa jumla ya mabao 3-2, ikishinda 2-1 Uw
WAZIRI MWIGULU AIOMBA YANGA IMUACHIE KAGOMA ACHEZEE SIMBA
- Get link
- X
- Other Apps
MLEZI wa klabu ya Singida Black Stars Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia ni Waziri wa Fedha na Mipango wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ameiomba klabu ya Yanga imruhusu kiungo Yusuph Ally Kagoma (28) aichezee Simba. Yanga imeweka pingamizi usajili wa Kagoma kutoka Singida Black Stars kwenda Simba, kwa sababu mchezaji huyo alisaini mkataba wao awali, lakini akaenda kusaini na kwa wapinzani pia. Waziri Nchemba, ambaye pia ni Mbunge wa jimbo la Iramba Magharibi, mkoani Singida kwa tiketi ya chama tawala, CCM amesema kwamba anafahamu undani wa suala la Yusuf Kagoma, lakini anaisihi Yanga imhurumie na kumruhusu acheze Simba ili kuokoa kipaji chake. "Nimewaomba viongozi wa Yanga wasamehe yote, waondoe shauri dhidi ya Kagoma, wamuache awe huru akaitumikie Simba kwa maslahi mapana ya mpira wa Tanzania na kwa faida ya mchezaji mwenyewe," amesema Waziri Nchemba kupitia ukurasa wake wa Instagram. Katika kufafanua sakata hilo, Waziri Nchemba amesema; "Ni kweli Ka
PAMBA SULUHU YA PILI MFULULIZO NYUMBANI LEO BAADA YA KUPANDA LIGI KUU
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Pamba Jiji FC imelazimishwa sare ya bila kufungana na Dodoma Jiji FC katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza. Hiyo inakuwa suluhu ya pili mfululizo nyumbani kwa Pamba iliyorejea Ligi Kuu msimu huu kufuatia kutoka sare ya 0-0 pia katika mchezo wa kwanza na Tanzania Prisons hapo hapo Kirumba.
ABUBAKAR BAKHRESA AKUTANA NA WACHEZAJI AZAM KUWATIA HAMASA WAING'OE APR
- Get link
- X
- Other Apps
MWENYEKITI wa Bodi ya Wakurugenzi ya Azam FC na Mkurugenzi Mkuu wa makampuni ya Bakhresa Group (SSB), Abubakar Said Salim Bakhresa mapema leo ametembelea kambi ya timu Jijini Kigali, Rwanda na kuzungumza na wachezaji kuelekea mchezo muhimu dhidi ya wenyeji, APR. Azam FC inatarajiwa kushuka Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali kuanzia Saa 1:00 usiku kumenyana na timu ya Jeshi la Watu wa Rwanda, APR katika mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika. Katika kikao hicho kilichohudhuriwa na viongozi wengine wa juu timu, akiwemo Mwenyekiti Nassor Idrisa 'Father', Abubakar amewataka wachezaji kujituma kuhakikisha wanaitoa APR na kufuzu hatua ya 32 Bora. Nao wachezaji wamemuahidi Abubakar watajtuma kuhakikisha wanapata matokeo mazuri dhidi ya wenyeji na kufuzu hatua inayofuata. Ikumbukwe mchezo wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 bao pekee la mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 56 kwa penalti kufuatia kiungo mzawa, Feisal Salum Abdal
MASHUJAA YAAMBULIA SULUHU KWA TZ PRISONS LAKE TANGANYIKA
- Get link
- X
- Other Apps
WENYEJI, Mashujaa FC wamelazimishwa sare ya bila mabao na jirani zao, Tanzania Prisons katika mchezo wa Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara leo Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma. Kwa matokeo hayo, Mashujaa inafikisha pointi nne baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Dodoma Jiji kweye mchezo wa kwanza, wakati Tanzania Prisons wanaokota pointi ya pili wakitoka kutoa sare nyingine ya bila mabao na Pamba Jiji Mwanza.
SIMBA QUEENS YATOA SARE, KUMENYANA NA POLISI YA KENYA NUSU FAINALI CECAFA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Simba Queens imekamilisha mechi zake za Kundi B Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa sare ya kufungana mabao 2-2 na PVP Buyenzi ya Burundi leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Mabao ya Simba Queens leo yamefungwa na nyota wake wa Kimataifa wa Kenya, kiungo Vivian Corazone Aquino Odhiambo Vivien na mshambuliaji Jentrix Shikangwa Milimu na kwa matokeo hayo wanamaliza na pointi saba na kuongoza Kundi B mbele ya Kawempe Muslim ya Uganda. Kawempe imemaliza na pointi sita baada ya ushindi wa 10-0 dhidi ya FAD ya Djibouti leo pia Uwanja wa Abebe Bikila, mabao yake yakifungwa na Hadijjah Nandago matano, Shadia Nabirye mawili, Rebecca Nakato, Halimah Kampi na Mary Kabucurezi moja kila mmoja. Sasa katika Nusu Fainali, Simba Queens watamenyana na washindi wa pili wa Kundi A, Polisi ya Kenya, wakati Kawempe Muslim watacheza na vinara wa Kundi A, wenyeji CBE FC Jumatatu.
RAIS SAMIA AONGEA NA WADAU WAWILI WAKUBWA NCHINI WAZIFADHILI SIMBA NA YANGA
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. Samia Suluhu Hassan amesema kwamba amezungumza na wadau wawili wakubwa nchini ili wazisaidie kiuchumi klabu za Simba na Yanga. Rais amesema hayo mapema leo wakati akiweka jiwe la Msingi wa ujenzi wa kituo cha Suluhu Sports Academy, Mkunguni – Kizimkazi, Zanzibar na kusema ujenzi wa kituo hicho utakaokamilika Aprili mwakani utasaidia kuzalisha vipaji zaidi vya vijana.
MAHOJIANO BIN ZUBEIRY NA NICO NJOHOLE
- Get link
- X
- Other Apps
ALIZALIWA Desemba 12, mwaka 1960, eneo la Chang’ombe Jijini Dar es Salaam, kabla ya kupata elimu yake ya Msingi katika shule ya Msimbazi Wavulana, baadaye sekondari ya Kinondoni Muslim Kidato cha kwanza pekee, akahamia Forodhani alikosoma hadi Kidato cha Nne. Wakati huo tayari alikwishakuwa mwanasoka maarufu kwenye vitongoji vya Jiji, akianzia timu za mitaa aliyoishi Chang’ombe na Ilala, baadaye Msimbazi Rovers ‘Pentagon’, kabla ya kujiunga na timu ya vijana ya Simba, maarufu kama Simba B. Kufuatia kundi kubwa la nyota wa Simba kutimkia Uarabuni wakiwemo viungo Haidari Abeid na Khalid Abeid, akawa miongoni mwa chipukizi waliopandishwa kikosi cha kwanza mwishoni mwa mwaka 1977 – wengine ni George Kulagwa, Rahim Lumelezi, Abbas Kuka. Alicheza Simba kwa mafanikio hadi mwaka 1982 alipoamua kwenda kucheza soka ya kulipwa Ulaya, akianzia England ambako pamoja na kukubalika kwenye klabu za AFC Bournemouth na Arsenal lakini ugumu wa kupata Hati ya Uhamisho wa Kimataifa, ITC ulimkwamisha. N
AZAM FC YAIFUATA APR USIKU HUU SHUGHULI NI JUMAMOSI AMAHORO
- Get link
- X
- Other Apps
KIKOSI cha Azam FC kinatarajiwa kuondoka Saa 9 usiku wa leo kwenda Kigali, nchini Rwanda kwa ajili ya mchezo wa marudiano Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya wenyeji, APR Jumamosi Uwanja wa Amahoro Jijini Kigali. Afisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria 'Zaka Zakazi' amesema timu inaondoka na wachezaji 22, huku wengine wakikosekana kwenye safari hiyo kipa Ali Ahamada, viungo Yahya Zayd, Sospter Bajana, Abdul Khamis Suleiman 'Sopu' na washambuliaji, Msenegal Alassane Diao na Mcolombia, Franklin Navarro kwa sababu ni majeruhi. Ikumbukwe mchezo wa kwanza Azam FC iliibuka na ushindi wa 1-0 bao pekee la mshambuliaji Mcolombia, Jhonier Alfonso Blanco Yus dakika ya 56 kwa penalti kufuatia kiungo mzawa, Feisal Salum Abdallah kuchezewa rafu kwenye eneo la hatari Jumapili. Mshindi wa jumla kati ya Azam ma APR atakutana na mshindi wa jumla kati ya JKU na Pyramids ya Mısri kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora. Pyramids iliichapa JKU 6-0 juzi Uwanja wa Jeshi
SIMBA QUEENS YAWAPIGA WAGANDA 3-0 NA KUTINGA NUSU FAINALI CECAFA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Simba Queens imefanikiwa kwenda Nusu Fainali ya Klabu Bingwa ya Wanawake Afrika Mashariki na Kati baada ya ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Kampe Muslim ya Uganda mchana wa leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa nchini Ethiopia. Mabao yote ya Simba Queens leo yamefungwa na nyota wake wa Kimataifa wa Kenya, mshambuliaji Jentrix Shikangwa Milimu dakika ya 54 na viungo Vivian Corazone Aquino Odhiambo dakika ya 69 na Elizabeth Wambui dakika ya 75. Kwa ushindi huo, Simba Queens inayofundishwa na wanasoka wa zamani wa kimtaifa wa kiume, Juma Mgunda na Mussa Mgosi inafikisha pointi sita na kuendelea kuongoza Kundi B kufuatia ushindi wa 5-0 dhidi ya FAD ya Djibouti kwenye mchezo wa kwanza juzi. Simba Queens, mabingwa wa micbhuano hiyo mwaka 2022 watakamilisha mechi zao za Kundi B kwa kumenyana na PVP Buyenzi ya Burundi hapo hapo Abebe Bikila. Kawemepe Muslim walioshinda 2-0 dhidi ya PVP Buyenzi katika mchezo wa kwanza wao watamaliza na FAD keshokutwa. Katika Kundi A wenyeji, CBE
SIMON MSUVA AONDOKA SAUDI ARABIA, AHAMIA LIGI KUU YA IRAQ
- Get link
- X
- Other Apps
KIUNGO mshambuliaji, Simon Happygod Msuva amejiunga na ya Al Talaba inayoshiriki ligi kuu ya Iraq akitokea Al Najmah ya Saudi Arabia. Personal information Full name Simon Happygod Msuva [ 1 ] Date of birth 2 October 1993 (age 30) Place of birth Dar es Salaam , Tanzania Height 1.75 m (5 ft 9 in) Position(s) Forward Senior career* Years Team Apps ( Gls ) 2010–2011 Azam FC 2011–2012 Moro United FC 2012–2017 Young Africans SC 2017–2020 Difaâ El Jadida 80 (28) 2020–2021 Wydad AC 37 (10) 2022–2023 Al-Qadsiah 28 (8) 2023 JS Kabylie 6 (0) 2024 Al-Najma 15 (4) International career ‡ 2012– Tanzania 90 (22)
ASHA MWALALA APIGA HAT-TRICK SIMBA QUEENS YASHINDA 5-0
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Simba Queens imeanza vyema michuano ya Klabu Bingwa Afrika Mashariki na Kati kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya FAD ya Djibouti katika mchezo wa Kundi B leo Uwanja wa Abebe Bikila mjini Addis Ababa, Ethiopia. Mabao ya Simba Queens yamefungwa na Jentrix Shikangwa dakika ya 24, Elizabeth Wambui dakika ya 30 na Asha Rashid ‘Mwalala’ matatu dakika ya 75, 80 na 89. Simba Queens itashuka tena dimbani Jumatano Saa 8:00 mchana kumenyana na Kawempe Muslim, kabla ya kukamilisha mechi zake za Kundi B kwa kucheza na PVP Buyenzi ya Burundi Ijumaa Saa 11:00 jioni hapo hapo Abebe Bikila. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
CHANGALAWE AMTWANGA BINGWA WA AFRIKA MKONGO KABEJI ADDIS ABABA
- Get link
- X
- Other Apps
BONDIA Yusuf Changalawe amefanikiwa kushinda pambano lake la usiku wa kuamkia leo na kufuta uteja mbele ya Bingwa wa Afrika Pita Kabeji kutoka DR Congo katika mapambano ya Usiku wa Mabingwa wa IBA yaliyofanyika katika ukumbi wa makumbusho wa Adwa, Mji mkuu wa Afrika Addis Ababa, Ethiopia. Pambano hilo lililokuwa na mvuto zaidi kati ya miamba hao wa Afrika katika uzani wa Light heavyweight 80kg, lilikuwa la tatu kukutana huku Changalawe akipoteza mara 2 dhidi ya Kabeji katika hatua ya nusu fainali ya mashindano ya Afrika Accra - Ghana 2023 na katika fainali ya mashindano ya Mandela Durban 2024 kwa matokea ya kutenganisha (Split decision) Changalawe aliyecheza kwa ustadi wa hali ya juu na kutumia akili nyingi alishinda kwa matokeo ya kutenganisha (split decision) katika pambano hilo la round nane (8) huku akishangiliwa zaidi na Waethiopia waliovutiwa na mchezo wake. "Ninamshukuru Mungu kwa ushindi wa leo, Nawashukuru IBA, AFBC na BFT kwa kunipa nafasi hii, hakika nimetimiza n
COASTAL UNION YACHAPWA 3-0 ANGOLA KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Coastal Union imejiweka njia panda katika michuano ya Kombe la Shirikisho Afrika baada ya kuchapwa mabao 3-0 na wenyeji, Bravos do Maquis jioni ya leo katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Uwanja wa Taifa wa Tundavala mjini Lubango nchini Angola . Timu hizo zitarudiana Agosti 25 Uwanja wa Azam Complex na mshindi wa jumla atakutana na St. Eloi Lupopo ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC). Wawakilishi wengine wa Tanzania katika Kombe la Shirikisho, Simba SC wataanzia Raundi ya Kwanza kwa kumenyana na mshindi kati ya Uhamiaji ya Zanzibar na Al Ahli Tripoli ya Libya.
DUBE, CHAMA NA AZIZ KI WAFUNGA YANGA YAWACHAPA VITAL'O 4-0 CHAMAZI
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA wa Tanzania, Yanga SC wametanguliza mguu mmoja hatua ya 32 Bora Ligi ya Mabingwa Afrika baada ya ushindi wa mabao 4-0 dhidi ya Vital'O ya Burundi katika mchezo wa kwanza Raundi ya Awali jioni ya leo Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam. Mabao ya Yanga leo yamefungwa na mshambuliaji Mzimbabwe, Prince Dube Mpumelelo dakika ya sita, kiungo Clatous Chotta Chama dakika ya 68, msambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 74 na kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki kwa penalti dakika ya 90'+1. Timu hizo zitarudiana Jumamosi ya Agosti 24 Uwanja wa Benjamn Mkapa, Dar es Salaam – na mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati Sports Club Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia.
PAMBA FC WAAMBULIA SULUHU KWA PRISONS UFUNGUZI LİGİ KUU
- Get link
- X
- Other Apps
YUSSUF BAKHRESA AFANYA KIKAO MAALUM NA WACHEZAJI AZAM FC
- Get link
- X
- Other Apps
SIMBA SC YAMTAMBULISHA MCAMEROON LEONEL ATEBA NI MNYAMA
- Get link
- X
- Other Apps
AZAM FC YASAJILI KİPA MWINGINE KUTOKA KVZ YA ZANZIBAR
- Get link
- X
- Other Apps
KLABU ya Azam FC imeimaridha safu yake ya ulinzi kwa kumsajili mlinda mlango, Arjif Ali Amour kutoka KVZ ya Zanzibar kwa mkataba wa mwana mmoja. Sasa Azam FC ina makipa watano, watatu wa kigeni, Msudan Mohamed Mustafa, Mghana Iddrisu Abdulai na Mcomoro, Ali Ahamada na mzawa mwingine mmoja, Zubery Foba.
KMC YARIDHIA UHAMISHO WA AWESU KWENDA SIMBA SC
- Get link
- X
- Other Apps
KLABU ya KMC imeridhia kiungo Awesu Ally Awesu ajiunge na Simba SC baada ya maridhiano kufuatia mazungumzo ya pande zote mbili. Simba ilimsajili Awesu, lakini KMC ikaweka pingamizi ikidai bado ina mkataba na kiungo huyo. Kamati ya Sheria na Hadhi za Wachezaji ikaelekeza Simba iwasiliane na KMC kwa ajili ya kufanya uhamisho wa mchezaji huyo. Jioni hii KMC imetoa taarifa ya kuridhia uhamisho wa Awesu baada ya kufikia maridhiano na Simba.
MBAPPE AFUNGA LA PILI REAL MADRID YATWAA UEFA SUPER CUP
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Real Madrid jana ilifanikiwa kutwaa taji la UEFA Super Cup baada ya ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya Atalanta Bergamo Uwanja wa Narodowy Jijini Warsaw, Poland. Mabao ya Real Madrid yalifungwa na kiungo wa Kimataifa wa Uruguay, Federico Valverde dakika ya 59 akimalizia pasi ya mshambuliaji Mbrazil, Vinícius Júnior na la pili, mshambuliaji mpya, Mfaransa Kylian Mbappé akimalizia pasi ya kiungo Muingereza, Jude Bellingham dakika ya 6 8. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
CHAMA NA MUSONDA WAFUNGA YANGA YASHINDA 4-1 MECHI YA KIRAFIKI KIGAMBONI
- Get link
- X
- Other Apps
KATIKA kujiandaa na mchezo wa kwanza Raundi ya Awali Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Vital’O ya Burundi Jumamosi Uwanja wa Azam Complex, Chamazi Jijini Dar es Salaam – Yanga jana ilicheza mechi ya kirafiki dhidi ya Green Warriors Uwanja w Avic Town, Kigamboni na kuibuka na ushindi wa 4-1. Mabao ya Yanga jana yalifungwa na Wazambia, Clatous Chama, Kennedy Musonda, Mkongo Jean Baleke na Mkenya, Duke Abya – na leo kikosi kinarejea mazoezini kujiandaa na mchezo wa Jumamoasi, ambao mechi zote mbili dhidi ya Vital’O zitachezwa Dar es Salaam, wa kwanza Yanga akiwa mgeni Chamazi na marudiano atakuwa mwenyeji Jumamosi ya Agosti 24 Uwanja wa Benjamn Mkapa, Dar es Salaam. Mshindi wa jumla atakutana na mshindi wa jumla kati SC Villa ya Uganda na Commercial Bank ya Ethiopia (CBE) katika Raundi ya kwanza kuwania kuingia hatua ya makundi, 16 Bora. GONGA KUTAZAMA PICHA ZAIDI
ADOLF MTASINGWA BITEGEKO ASAINI MKATABA MPYA AZAM FC HADI 2027
- Get link
- X
- Other Apps
KIUNGO Adolf Mtasingwa Bitegeko (24) amesaini mkataba mpya wa miaka miwili kuendelea na majukumu Azam FC hadi mwaka 2027. Adolf ni miongoni wachezaji waliopikwa katika akademi ya Azam FC, kabla ya mwaka Machi 2019 kwenda Icenald kujiunga na KR Reykjavík hadi mwaka Oktoba mwaka huo akaenda Keflavík, Juni 1, 2020 akarejea KR Reykjavík, kabla ya kujiunga na Völsungur ÍF Februari mwaka 2021 ambako alipiga kazi hdi Janauri mwaka huu akarejea Azam FC.
YANGA WAICHAPA AZAM FC 4-1 NA KUTWAA NGAO YA JAMII
- Get link
- X
- Other Apps
MABINGWA wa Tanzania, Yanga wamefanikiwa kutwaa Ngao ya Jamii baada ya kutoka nyuma na kushinda mabao 4-1 dhidi ya Azam FC usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Azam FC walitangulia kwa bao la kiungo mzawa Feisal Salum dakika ya 13, akimalizia krosi ya winga Mgambia, Gibril Sillah kutoka kulia kumchambua kipa namba moja wa Mali, Djigui Diarra. Yanga ikazinduka kwa mabao ya mshambuliaji Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo dakika ya 19, beki Mmali, Yoro Mamadou Diaby aliyejifunga dakika ya 28, kiungo Mburkinabe, Stephane Aziz Ki dakika ya 31 na mshambuliaji mzawa, Clement Francis Mzize dakika ya 90’+1. Mapema katika mchezo wa kusaka mshindi wa tatu, bao Saleh Karabaka Kikuya dakika ya 11 liliipa Simba SC ushindi wa 1-0 dhidi ya Coastal Union hapo hapo Uwanja wa Benjamin Mkapa.
TANZANIA YAHITIMISHA ‘SALAMA’ USHIRIKI USHIRIKI WAKE OLIMPIKI YA PARIS
- Get link
- X
- Other Apps
TANZANIA imehitimisha ushiriki wake kwenye Michezo ya Olimpiki ya mwaka huu bila kushinda Medali yoyote baada ya Wanariadha wake, Jackline Juma Sakilu na Magdalena Crispin Shauri kufanya vibaya kwenye Marathoni ya Wanawake katika kilele cha Michezo hiyo iliyoanza Julai 26. Magdalena Crispin Shauri amemaliza nafasi ya 40 Kati ya wakimbiaji 80 waliomaliza, akitumia muda wa Saa 2 dakika 31 na sekunde 58, wakati Jackline Juma Sakilu ni kati ya wanariadha 11 ambao hawakumaliza mbio hizo. Mholanzi mwenye asili ya Ethiopia, Sifan Hassan ameshinda Medali ya Dhahabu kwenye Marathoni hiyo akiweka rekodi kwa kutumia muda wa Saa 2 dakika 22 na sekunde 55, akifuatiwa na Tigst Assefa wa Ethiopia na Hellen Obiri wa Kenya katika nafasi ya tatu leo Jijini Paris. Ikumbukwe jana wakimbiaji wengine wawili wa Tanzania, Alphonce Felix Simbu na Gabriel Gerald Geay walikimbia Marathoni ya wanaume, ambayo Tamirat Tola wa Ethiopia alishinda Medali ya Dhahabu. Angalau Simbu alimaliza nafasi ya 17 akitumia muda
SIMBA SC WASHINDI WA TATU NGAO YA JAMII, COASTAL YAFA 1-0
- Get link
- X
- Other Apps
AZAM FC YAAJIRI KOCHA MPYA KUTOKA EL MAREEIKH YA SUDAN
- Get link
- X
- Other Apps
ARAJIGA APEWA AZAM NA YANGA, KAYOKO COASTAL NA SIMBA KESHO
- Get link
- X
- Other Apps
REFA mwenye beji ya Shirikisho la Soka la Kimataifa (FIFA), Ahmed Arajiga ndiye atakayechezesha Fainali ya Ngao ya Jamii baina ya Azam FC na Yanga SC kesho kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Arajiga Refa Bora wa msimu atasaidiwa na Frank Komba wa Dar es Salaam na Mohamed Mkono wa Tanga, wakati mezani atakuwepo Amina Kyando wa Morogoro na Mtathmini wa mchezo ni Refa Mstaafu wa FIFA, Soud Abdi wa Arusha. Mchezo wa kusaka mshindi wa tatu baina ya Coastal Union na Simba utakaochezwa kesho Saa 10:00 jioni hapo hapo Uwanja wa Mkapa utachezeshwa na Ramadhani Kayoko atakayesaidiwa na Glory Tesha, wote wa Dar es Dalaam na Hamdan Said wa Mtwara. Refa wa akiba kwenye mchezo huo atakuwa Isihaka Mwalile wa Dar es Salaam na Mtathmini wa mechi hiyo ni Refa Mstaafu wa FIFA pia, Isaro Chacha wa Mwanza.
RAIS WA ZAMANI WA CAF ISSA HAYATOU AFARIKI DUNIA
- Get link
- X
- Other Apps
RAIS wa zamani wa Shirikisho la Soka Afrika (CAF), Mcameroon Alhaj Issa Hayatou, amefariki dunia jana Jijini Paris nchini Ufaransa akiwa na umri wa miaka 77. Rais wa Shirikisho la Soka Cameroon (FECAFOOT), Samuel Eto'o amesema leo kwamba Hayatou amefariki Saa 24 kabla ya kutimiza miaka 78 kufuatia kuugua nchini humo. Mapema jana Rais wa FIFA, Gianni Infantino alitoa taarifa za kifo cha Hayatou kupitia ukurasa wake wa Instagram: "Nimehuzunishwa kusikia kifo cha rais wa zamani wa CAF, rais wa zamani wa FIFA na muda mfupi, makamu wa rais wa FIFA na mjumbe wa Baraza la FIFA Issa Hayatou,". "Akiwa shabiki wa michezo, alijitolea maisha yake kwa michezo. kwa niaba ya FIFA, rambirambi ziende kwa familia yake, marafiki, wafanyakazi wenzake wa zamani na wote wanaomfahamu wapumzike kwa amani,". Hayatou pia alikuwa Mjumbe wa Kamati ya Kimataifa ya Olimpiki (IOC) kwa miaka 15, hadi 2016, na alibaki kuwa Mjumbe wa heshima. Ingawa alikuwa mwanariadha nyota enzi zake,
SIMBA NA YANGA NYINGINE JUMAMOSI YA OKTOBA 19 LİGİ KUU
- Get link
- X
- Other Apps
LIGI Kuu ya NBC Tanzania Bara inatarajiwa kuanza rasmi Agosti 16, Uwanja wa CCM Kirumba Jijini Mwanza ukipewa heshima ya ufunguzi kwa mchezo baina ya wenyeji, Pamba Jiji FC dhidi ya Tanzania Prisons kuanzia Saa 10:00 jioni. Vigogo, Simba watashuka dimbani Agosti 18 kumenyana na Tabora United kuanzia Saa 10:15 jioni Uwanja wa Manispaa ya Kinondoni, KMC Complex, Dar es Salaam. Azam FC watacheza mechi yao ya kwanza Agosti 28 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Meja Jenerali Mstaafu Isamuhyo, Mbweni, Dar es Salaam. Mabingwa watetezi, Yanga wao wataanzia Bukoba Agosti 29 kumenyana na wenyeji, Kagera Sugar kuanzia Saa 1:00 usiku Uwanja wa Kaitaba. Watani wa jadi watakutana katika mechi ya mzunguko wa kwanza Jumamosi ya Oktoba 19, Simba akiwa mwenyeji na marudiano yatafuatia Jumamosi pia ya Machi 1, Mwaka 2025. GONGA HAPA KUTAZAMA RATIBA KAMILI YA LİGİ KUU
MAXI MPIA NZENGELI AIPELEKA YANGA FAINALI NGAO YA JAMII...MNYAMA CHALI ILE YENYEWE
- Get link
- X
- Other Apps
KLABU ya Yanga imefanikiwa kutinga Fainali ya Ngao ya Jamii kwa ushindi wa 1-0 dhidi ya watani, Simba katika mchezo wa Nusu Fainali usiku huu Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Pongezi kwa mfungaji wa bao hilo pekee, kiungo Mkongo, Maxi Mpia Nzengeli dakika ya 44 akimalizia pasi nzuri ya mshambuliaji mpya, Mzimbabwe Prince Dube Mpumelelo. Sasa Yanga watakutana na Azam FC katika Fainali itakayopigwa Jumapili hapo hapo Uwanja wa Mkapa kuanzia Saa 1:00 usiku ikitanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu itakayoanza Saa 10:00 jioni. Azam FC imetinga Fainali kwa ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Mabao ya Azam yamefungwa na winga Mgambia Gibril Sillah dakika ya 13, kiungo Feisal Salum dakika ya 40, washambuliaji Mcolombia Jhonier Blanco dakika ya 45'+1, Adam Omary dakika ya 87 na kiungo Mcolombia, Ever William Meza Mercado dakika ya 90'+2. Kwa upande wao, Coastal Union ambayo itakutana na Simba Jumap
AZAM FC YAITANDIKA COASTAL 5-2 NA KUTINGA FAINALI NGAO YA JAMII
- Get link
- X
- Other Apps
TIMU ya Azam FC imefanikiwa kuingia Fainali ya michuano ya Ngao ya Jamii baada ya ushindi wa mabao 5-2 dhidi ya Coastal Union jioni ya leo Uwanja wa New Amaan Complex, Zanzibar. Mabao ya Azam yamefungwa na winga Mgambia Gibril Sillah dakika ya 13, kiungo Feisal Salum dakika ya 40, washambuliaji Mcolombia Jhonier Blanco dakika ya 45'+1, Adam Omary dakika ya 87 na kiungo Mcolombia, Ever William Meza Mercado dakika ya 90'+2. Kwa upande wao, Coastal Union mabao yao yamefungwa na kiungo Charles Semfuko dakika ya 27 na Abdallah Hassan dakika ya 85. Sasa Azam FC itakutana na mshindi wa Nusu Fainali ya Pili baina ya watani wa jadi, Simba na Yanga ambazo zipo dimbani Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam zinapapatuana kusaka tiketi ya Fainali – itakayochezwa Jumapili ikitanguliwa na mechi ya kusaka mshindi wa tatu.
MECHI YA WATANI LEO; TUTAINGIA NA MBINU TOFAUTI, ASEMA KOCHA WA SIMBA SC
- Get link
- X
- Other Apps
KOCHA Mkuu wa Simba SC, Fadluraghman 'Fadlu' Davids amesema kwamba ataingia na mbinu tofauti kuhakikisha anapata matokeo mazuri dhidi ya watani, Yanga leo Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam. Akizungumza katika mkutano na Waandishi wa Habari jana Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es Salaam, Davids amesema analazimika kufanya hivyo kutokana na uzoefu wake wa mechi za wapinzanina yeye timu yake ni mpya. "Tunaichukulia hii mechi kama nyingine, tunahitaji kushinda ili kuanza vizuri msimu kwa kulitetea Kombe hili. Nina uzoefu wa michezo hii mikubwa ya wapinzani, ukiangalia timu yetu ni mpya, tutakuja na mbinu tofauti kuhakikisha tunapata matokeo mazuri,"amesema raia huyo wa Afrika Kusini. Kwa upande wake Nahodha wa timu hiyo, Mohamed Hussein 'Tshabalala' amesema kwamba utakuwa mchezo wenye ushindani kwa sababu wanakwenda kukutana na timu yenye wachezaji wazuri, ila malengo yao ni kupata ushindi. "Kulingana na maandalizi tuliyoyafanya, timu
MASHABIKI WANANE KUULA PARIMATCH ‘SAFARİ YA BATA’ DUBAİ
- Get link
- X
- Other Apps
Meneja Masoko wa kampuni ya michezo ya kubashiri ya Parimatch , Levis Paul ( wa pili kulia ) akizungumza wakati wa uzinduzi wa promosheni ya Dubai Kumenoga iliy ozi n duliwa kwa kushirikiana na kampuni ya ya simu ya Airtel kupitia huduma za Airtel Money ambapo jumla ya washindi nane watashinda tiketi na kupata fursa ya kutembelea nchini Dubai. Wa kwanza kulia ni balozi wa kampuni ya Parimatch , Haji Manara na maofisa wengine wa Airtel ambao ni , George Majumba ( wa tatu kushoto ), Chakicha Mshana ( wa pili kushoto ) na balozi wa Parimatch , Ester Luckson maarufu kwa jina la Mama Chanja wa kwanza kushoto . MASHABIKI wa nane wa soka watapara fursa ya kutembelea nchi ni Dubai endapo watashinda tiketi kupitia promosheni ya Dubai Kumenoga iliyoziduliwa na k ampuni ya michezo ya kubahatisha Parimatch kwa